Vijana wa kiume wanaotumia picha za utupu kufanya utapeli

Walipopelekwa Marekani, walikiri kosa na wanasubiri hukumu.

Muhtasari
  • Jordan DeMay alifariki mwaka 2022 baada ya ndugu wawili Samuel na Samson Ogoshi, kutoka Logos, Nigeria, kupata picha zake za utupu baada ya kujifanya msichana mrembo wa rika lake, na kutishia kumchafua kwa kutuma picha hizo za uchi kwenye mtandao.

Mvulana wa kiume alijiua saa sita tu baada ya 'walaghai' kutishia kuchapisha picha zake za utupu kwenye mitandao.

Jordan DeMay alifariki mwaka 2022 baada ya ndugu wawili Samuel na Samson Ogoshi, kutoka Logos, Nigeria, kupata picha zake za utupu baada ya kujifanya msichana mrembo wa rika lake, na kutishia kumchafua kwa kutuma picha hizo za uchi kwenye mtandao.

Mama yake DeMay, Jenn Buta, sasa anatumia ukurasa wa TikTok wa mwanawe kuwaonya vijana kuhusu wahalifu kama hao, ambao wameenea nchini Nigeria - na video zake zimetazamwa zadi ya mara milioni moja.

Polisi wa Nigeria waliambia BBC, madai kuwa hawalichukulii suala hilo kwa uzito ni ya "ujinga."

Vijana hao wa miaka 22 na 20 walitumiana picha na mazungumzo ya mapenzi na kijana huyo wa miaka 17 kwenye Instagram, walimtumia picha za uchi kabla ya kumfanya nae atume picha zake akiwa uchi.

Kisha, walimtishia kumchafua asipowapa pesa ili wasizichapishe picha hizo kwenye mtandao.

Jordan alipowaambia hawezi tena kuwatumia pesa na atajiua, vijana hao walisema: "Afadhali ufanye hivyo haraka - au tutakufanya ufanye."

Walipopelekwa Marekani, walikiri kosa na wanasubiri hukumu.

"Ilikuwa chini ya saa sita tangu Jordan alipoanza kuzungumza nao hadi alipojiua," Jenn aliambia BBC, kutoka nyumbani kwake huko Michigan, kaskazini mwa Marekani.