Waogeleaji watatu wajeruhiwa katika mashambulizi ya papa

Mwanamke mmoja alisemekana kukatwa sehemu ya mkono wake baada ya kuumwa.

Muhtasari

•Mmoja wa wasichana alipata "majeraha makubwa kwenye sehemu ya juu ya mguu na mkono mmoja."

•Sehemu ya mkono wake ulilazimika kukatwa, mkuu wa zimamoto Ryan Crawford baadaye aliambia mkutano wa habari

Image: BBC

Watu wanaotembelea fukwe za Florida wameshauriwa kuwa makini, baada ya waogeleaji watatu kushambuliwa na papa katika mashambulizi mawili tofauti.

Mwanamke mmoja alisemekana kukatwa sehemu ya mkono wake baada ya kuumwa siku ya Ijumaa katika Kaunti ya Walton kaskazini-magharibi mwa Florida.

Chini ya saa mbili baadaye, katika ufuo mwingine wa maili nne zaidi mashariki, wasichana wawili waliokuwa kwenye maji hadi kiunoni na marafiki walishambuliwa.

Mmoja wa wasichana hao alipata "majeraha makubwa kwenye sehemu ya juu ya mguu na mkono mmoja" huku mwingine akiwa na majeraha madogo kwenye mguu wake mmoja, maafisa wa zima moto walisema.

Mamlaka zimekuwa zikishika doria kwenye ufuo kwa boti na baadhi ya fuo zilifungwa, ingawa zilifunguliwa tena Jumamosi na bendera za zambarau zikionya juu ya viumbe hatari vya baharini.

Tukio la kwanza lilitokea mwendo wa saa 13:20 kwa saa za huko siku ya Ijumaa wakati mwanamke, mwenye umri wa miaka 45, alishambuliwa karibu na WaterSound Beach, Wilaya ya Kusini ya Walton Fire ilisema.

Alipata "majeraha mabaya" kwenye nyonga na chini ya mkono wake wa kushoto na alipelekwa hospitalini kwa ndege, maafisa wa zima moto walisema.

Sehemu ya mkono wake ulilazimika kukatwa, mkuu wa zimamoto Ryan Crawford baadaye aliambia mkutano wa habari, kulingana na mshirika wa BBC wa Marekani CBS News