Hamas yakubali mazungumzo na Israel ili kusitisha vita Gaza

Misri na Qatar zimesema zitahakikisha Hamas wanashiriki mazungumzo wakati Marekani imesema itashirikisha Israel

Muhtasari

• Hamas inasema inakaribisha kupitishwa kwa azimio hilo lililoandaliwa na Marekani, ambalo linaelezea mpango wa awamu tatu wa kusitisha mapigano.

• Mwanachama mmoja tu wa baraza la usalama - Urusi - hakuipigia kura hoja hiyo

Machafuko ya vita Gaza
Image: HISANI
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha azimio lake la kwanza la kuunga mkono mpango wa kusitisha mapigano unaolenga kumaliza vita kati ya Israel na Hamas.
 
Azimio hilo lililoandaliwa na Marekani linaweka wazi mpango wa awamu tatu wa kusitisha mapigano, ambao Rais wa Marekani Joe Biden aliuelezea kama mpango wa Israel - ingawa jinsi utakavyokuwa na ufanisi unabakia wasiwasi.
 
Ikijibu azimio hilo, Hamas ilisema iko tayari kushirikiana na wapatanishi katika kutekeleza kanuni za mpango huo.
 
Kabla ya kura hiyo, Benjamin Netanyahu alisema Rais Biden aliwasilisha sehemu kiduchu mno  za pendekezo hilo.
 
Mpango wa awamu ya tatu wa kusitisha mapigano unatoa wito wa kuachiliwa kwa mateka zaidi na kusitishwa kwa muda kwa mapigano ambayo yatadumu kwa muda mrefu.
 
Mazungumzo ya awamu ya pili yanalenga kuachiliwa kwa mateka wote, kujiondoa kikamilifu kwa vikosi vya Israeli kutoka Gaza na kukomesha kabisa uhasama.
 
Awamu ya tatu inatoa wito wa kujengwa upya kwa Gaza ambayo ni azimio la kwanza kupitishwa na baraza linalounga mkono mpango mahususi wa kusitisha mapigano.
 
Kati ya mataifa 15 kwenye baraza hilo, 14 yaliunga mkono hoja hiyo siku ya Jumatatu, huku Urusi ikisusia. Tunasubiri Hamas kukubaliana na makubaliano ya kusitisha mapigano hayo kulingana na  balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield.
 
"Kwa kila siku inayopita, mateso yasiyo ya lazima yanaendelea," bi Thomas-Greenfield alisema.
 
Misri na Qatar zimeihakikishia Washington kuwa zinafanya kazi kuhakikisha Hamas inashiriki mazungumzo ya kusitisha mapigano, wakati Marekani itahakikisha Israel "inatimiza wajibu wake pia".
 
Balozi wa Uingereza Barbara Woodward alisema azimio hilo ni hatua muhimu kuelekea kumaliza mzozo huo.
 
"Hali ya Gaza ni janga na mateso yameendelea kwa muda mrefu sana," alisema, na kuongeza kuwa makubaliano yaliyowasilishwa ni jambo ambalo Uingereza imekuwa ikitaka kwa muda mrefu.