Vyama 5 vya kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Serikali ya umoja imedhamiria kuangazia uchumi,uundaji wa nafasi za kazi pamoja na miradi nyingine.

Muhtasari

•Jumla ya vyama vitano vimejiunga pamoja na ANC kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ya Afrika Kusini baada ya tangazo na ANC siku ya Jumatatu 17,Juni 2024.

•Kiongozi wa ANC,Cyril Ramaphosa alichguliwa tena kuwa rais wa Afrika Kusini na bunge siku ya Ijumaa 14.

Ramaphosa.
Ramaphosa.
Image: Twitter

Jumatatu, Chama cha African National Congress (ANC) kilisema kuwa vyama vitano vya kisiasa vimetia saini rasmi taarifa ya nia ya kushiriki katika serikali ya umoja wa kitaifa (GNU).

Kufuatia uchaguzi wa mwezi uliopita, ANC ililazimika kutengeneza ushirikiano na vyama vingine vya kisiasa baada ya kushindwa kupata wingi wa wabunge kwa mara ya kwanza tangu uchaguzi wa 1994.

Kiongozi wa ANC Cyril Ramaphosa alichaguliwa tena kuwa rais wa Afrika Kusini na bunge siku ya Ijumaa 14 Juni, huku chama chake kikipata uungwaji mkono kutoka kwa mpinzani wake mkubwa.Miongoni mwa vyama vilivyojiunga ni pamoja na  kile kinachoongozwa na wazungu,"The White-led"  kinachounga mkono biashara cha Democratic Alliance, pamoja na vyama viwili vidogo - Inkatha Freedom Party na Patriotic Alliance.

Aidha, chama cha ANC kilisema Jumatatu kuwa chama kingine kidogo cha 'GOOD'  pia kimejiandikisha kuwa sehemu ya mkataba wa serikali ya umoja.

ANC ilisema serikali ya umoja itahakikisha uwakilishi katika serikali kwa vyama vyote vinavyoshiriki na itafanya maamuzi kwa maafikiano.

Miongoni mwa vipaumbele vyake, serikali ya umoja imedhamiria kuangazia ukuaji wa haraka, shirikishi na endelevu wa uchumi, kukuza uwekezaji wa mtaji wa kudumu, uundaji wa nafasi za kazi, mageuzi ya ardhi na maendeleo ya miundombinu.

"Rais atatumia mamlaka ya kuteua baraza la mawaziri, kwa kushauriana na viongozi wa vyama vya GNU (serikali ya umoja wa kitaifa), kwa kuzingatia itifaki zilizopo kuhusu maamuzi na bajeti ya serikali," ANC ilisema, na kuongeza kuwa bado iko kwenye majadiliano na vyama vingi kujiunga na serikali.