Wanafunzi walazwa hospitalini kwa kula vibanzi vyenye 'pilipili nyingi'

Takriban wanafunzi 30 walikula vibanzi hivyo baada ya mmoja wao kuja nazo shuleni.

Muhtasari

•Wanafunzi kumi na wanne wa shule ya upili huko Tokyo walikimbizwa hospitalini baada ya kula vibanzi "vyenye pilipili nyingi.

Image: BBC

Wanafunzi kumi na wanne wa shule ya upili huko Tokyo walikimbizwa hospitalini baada ya kula vibanzi "vyenye pilipili nyingi", polisi walisema.

Takriban wanafunzi 30 walikula vibanzi hivyo baada ya mmoja wao kuja nazo shuleni, vyombo vya habari vya nchini humo viliripoti.

Muda si muda, baadhi yao walianza kulalamika kuwa na kichefuchefu na maumivu makali mdomoni, na kusababisha idara ya zimamoto na polisi kupigiwa simu.

Wasicha 13 na mvulana mmoja ambao walipelekwa hospitali walikuwa wamepoteza fahamu.

Kampuni inayotengeneza kitafunio hicho, Wanafunzi kumi na wanne wa shule ya upili huko Tokyo walikimbizwa hospitalini baada ya kula vibanzi "vyenye pilipili nyingi., alitoa taarifa akiomba radhi kwa "tatizo lolote" kwa wateja, na kuwatakia wanafunzi afueni ya haraka.

Shule na kampuni bado hazijasema lolote tangu BBC ilipowasiliana nazo.

Tovuti ya kampuni hiyo inaonya yeyote ambaye angependa kula vibanzi hivyo.

Pia, " inakataza wale walio na umri chini ya miaka 18 kutokula vibanzi hivyo ambavyo vina pilipili sana – na wale ambao wanapenda kula vyakula vya pilipili "kula kwa tahadhari". Vibanzi hivyo vina pilipili kiasi kwamba vinaweza kusababisha maumivu", ilisema.

Pia, kampuni hiyo inashauri watu kutokula vibanzi hivyo "wakiwa peke yao" na kuongeza kuwa zinaweza kusababisha kuhara zikiliwa "kwa wingi".