Watu wanne wauawa katika kisa cha kufyatuliwa risasi Marekani

Idadi nyingine ya watu ambayo haijabainishwa wanazidi kupokea matibabu ya majeraha ya risasi.

Muhtasari

• Visa vya raia kufyatuliwa marisasi na majambazi vimeongezeka na kufikia Septemba angalau visa 385 vilikuwa vimeripotiwa.

• Watu wanne waliaga dunia katika kisa cha punde zaidi cha Jumamosi jioni

Crime Scene
Image: HISANI

Watu wanne wamefariki na idadi ya watu wengine ambayo haijawekwa wazi wamepata majeraha katika kisa ambapo watu wasiojulikana waliwafyatulia raia marisasi.

Kisa hicho  kilitukia siku ya Jumamosi jioni katika eneo la Birmingham, jimbo la Alabama nchini Marekani.

Afisa wa police kwa jina Truman Fitzgerald alisema kuwa idadi ya watu  isiyojulikana na ambao walikuwa wamejihami kwa bunduki walifyatua marisasi kwa kundi la watu na kuua watu wanne na kujeruhi wengine kadhaa.

Kulingana na watu walioshuhudia kisa hicho waliozungumza na kituo kimoja cha habari katika jimbo hilo. milio ya risasi iliyosikika ilitoa sauti za kana kwamba bunduki iligeuzwa kuwa otomatiki.

Hata hivyo,kikosi cha polisi kinaendeleza uchunguzi wa kubaini ikiwa washambulizi walitumia gari au la.

Mwaka huu pekee shirika la habari la kimataifa BBC mnamo tarehe 5 Septemba, liliripoti kuwa takribani visa 385 vya raia kufyatuliwa risasi vilirekodiwa nchini Marekani.

Aidha kutokana na kisa cha Jumamosi, majeruhi wanne wako katika hali mbaya ya kiafya wengine wakitibiwa majeruhi madogo ya risasi.