Wizara ya afya ya Lebanon inasema 558 wameuawa tangu mashambulizi ya Jumatatu

Waziri wa afya wa Lebanon Firass Abiad anasema kati ya waliouawa, 50 walikuwa watoto.

Muhtasari

•Akizungumza katika mkutano na wanahabari, amesema wanahabari "sekta ya afya inahitaji msaada wetu".

Ndege ya kivita
Image: BBC

Katika taarifa zao za hivi punde, wizara ya afya ya Lebanon inasema watu 558 wameuawa tangu Jumatatu baada ya mashambulio ya Israel nchini humo.

Waziri wa afya wa Lebanon Firass Abiad anasema kati ya waliouawa, 50 walikuwa watoto.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari, amesema wanahabari "sekta ya afya inahitaji msaada wetu".

"Tunatumai kinachokuja sio kibaya zaidi. Tutaendelea kutekeleza jukumu letu.

"Wahudumu wa matibabu wanne walifariki jana wakati magari ya kubebea wagonjwa na gari la kubebea wagonjwa vilipopigwa na kombora la Israel. Asubuhi ya leo waliiga kombora hospitali ya Bint Jbail," Abiad anasema.

Itakumbukwa kuwa Jumatatu ilikuwa siku mbaya zaidi ya mashambulizi nchini Lebanon tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mnamo 1990.