Mahakama yaahirisha kesi ya mauaji ya ndugu wa Kianjakoma

"Walikuwa wavulana wazuri sana wenye bidii na wachapakazi," Ndwiga alisema

Muhtasari
  • Mahakama ilikuwa tayari imesikiliza ushahidi kutoka kwa marafiki wawili wa ndugu hao na wazazi wao
Mahakama
Mahakama
Image: MAHAKAMA

Kesi ya mauaji ya ya ndugu wa Kianjakoma ambayo ilipaswa kusikizwa leo imeahirishwa hadi tarehe isiyojulikana kufuatia uhamisho wa hakimu wa mahakama hiyo.

Kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa na Jaji Daniel Ogembo lakini japo kesi hiyo iliorodheshwa leo katika mahakama yake haikuendelea kutokana na uhamisho wake.

Katika kesi hiyo, maafisa sita Benson Mputhia, Consolata Kariuki, Nicholas Cheruyoit, Martin Wanyama, Lilian Chemuna na James Mwaniki wameshtakiwa kwa mauaji ya Benson na Emmanuel Ndwiga.

Mahakama ilikuwa tayari imesikiliza ushahidi kutoka kwa marafiki wawili wa ndugu hao na wazazi wao na mashahidi zaidi walitarajiwa kutoa ushahidi leo.

Washtakiwa hao walielezwa kuwa watapewa tarehe mpya kwa notisi na mahakama ili waweze kufika kwa kutajwa. Mnamo Novemba mwaka jana, wazazi wa ndugu wa marehemu walisimulia korti kwa hisia jinsi walivyogundua kuwa wana wao walikufa mikononi mwa polisi mnamo 2021.

John Ndwiga na Catherine Gichuki waliambia mahakama simu za mwisho walizopigia marehemu kabla ya kupatikana wakiwa wamefariki.

Baba huyo aliwataja wavulana hao kuwa wazuri sana, akisema hawakuwahi kulala nje ya nyumba tangu siku walipozaliwa.

"Walikuwa wavulana wazuri sana wenye bidii na wachapakazi," Ndwiga alisema