Hiziri ya mganga kukosa kufanya kazi na mrembo wako kula nauli si kesi ya Mahakama

"Ninawahurumia wanaume wanaopoteza pesa kwa wapenzi ambao hula nauli yao lakini wanashindwa kuheshimu mialiko" - hakimu alisema.

Muhtasari

• "Hirizi zinaposhindwa kufanya kazi baada ya kulipia huduma, ukitaka pesa zako zirudishwe tu na mganga wako,” - Hakimu alisema.

Tabitha Wanjiku Mbugua, hakimu mkaazi wa mahakama za madai madogo ya Eldoret.
Tabitha Wanjiku Mbugua, hakimu mkaazi wa mahakama za madai madogo ya Eldoret.
Image: Screengrab,

Hakimu Mkazi Mwandamizi na mwamuzi wa Mahakama ya Madai Ndogo ya Eldoret Tabitha Wanjiku Mbugua amesema kuwa katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na murndiko wa kesi za kushangaza ambazo zinaandikishwa katika mahakama za madai madogo.

Katika video moja ambayo alionekana akihutubia watu kwenye mkutuano mmoja, Mbugua anasikika akisema kuwa mahakama hizo hazisuluhishi kesi za mwanamume kumtumia mpenzi wake nauli ya kumtembelea na mpenzi wake kukosa kufika.

Pia alibainisha kwamba kesi za mtu kwenda kwa mganja ili kufanyiwa tambiko na matokeo yake yashindwe kutokea kama alivyoaidiwa baada ya ramli, hiyo si kesi ya mahakamani.

“Ninawahurumia wanaume wanaopoteza pesa kwa marafiki zao wa kike ambao hula nauli yao lakini wanashindwa kuheshimu mialiko. Baadhi ya wanaume hawa wameenda kwa mahakama yangu ili kupata usaidizi lakini, kwa bahati mbaya, mahakama yangu haiwezi kuwalazimisha wanawake kama hao kulipa nauli. Sheria ya mamlaka ya mahakama ndogo za madai hainiruhusu kutoa uamuzi kuhusu hilo,” alisema.

“Hizi kesi za kudai kuwa ulimlipa mganga na hirizi hazikufanya kazi haziwezi kudaiwa katika mahakama yetu. Hirizi zinaposhindwa kufanya kazi baada ya kulipia huduma, ukitaka pesa zako zirudishwe tu na mganga wako,” aliongeza hakimu huyo.

Hata hivyo, aliendelea kutolea mifano ya kesi ambazo mahakama za madai madogo zinafaa kushughulikia ikiwemo mikopo ya haraka kwa rafiki yako ambaye amekataa kulipa, hiyo atakusaidia kuishughulikia.

Aliwashauri watu wenye kesi ndogo ndogo kama hizo kumtafuta na atakuwa radhi kutoa mwelekeo jinsi ya kujaza fomu za kufungua kesi hizo, huku pia akitoa wito kwa wale walioshindwa kurudisha madeni kama hayo kumfikia ili kuwapa taratibu za kuweza kurudisha madeni hayo pasi na kufikia faini.