Mama wa mvulana ambaye korodani zake ziliharibiwa na walimu 5 kwa kipigo alia kortini - video

Katika video hiyo, mama aligeuka mbogo akiuliza mbona mwalimu mmoja tu asingemuadhibu mwanawe badala ya walimu watano kushirikiana kwa mtoto wa miaka 12 tu ambaye ni uzao wake wa pekee.

Muhtasari

• “Kuna mtu alitaka kuniibia mtoto wangu pekee wa uzao, walimu wakubwa walitaka aache kuzaa" - mama alilia.

Mama wa mtoto aliyevunjwa korodani alia kortini
Mama wa mtoto aliyevunjwa korodani alia kortini
Image: Screengrab

Mahakama moja mjini Kakamega ilishuhudiwa simanzi na jitimai baada ya mama wa mvulana aliyeharibiwa kodorani zake kutokana na kichapo cha walimu watano shuleni mwaka 2021 kuelezea ushahidi wake kwa kilio.

Mwanamke huyo alizidiwa na hisia wakati akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo ambapo walimu hao watano wanadaiwa kumshambulia mtoto huyo na kumuacha akiuguza majeraha sehemu zake za siri.

Mvulana huyo aliadhibiwa viboko baada ya kuripotiwa kupatikana na simu ya mkononi akiwa shuleni Oktoba 19, 2021.

Caroline Khamali, ambaye pia ni mwalimu katika shule tofauti, alijikuta akiangua kilio na kulia mahakamani kutokana na aina ya adhabu aliyopewa mtoto wake na walimu wa shule hiyo.

“Mwalimu mmoja alitosha kumwadhibu kijana huyo kwa kosa lolote alilofanya, ikiwa ni pamoja na kuwa na simu shuleni. Kumpiga kwenye kundi la wafanyakazi na hasa kulenga uanaume wake ilikuwa ni makosa,” alisema.

“Kuna mtu alitaka kuniibia mtoto wangu pekee wa uzao, walimu wakubwa walitaka aache kuzaa, niambieni mahakama, kwa nini mtu mzima amfanyie hivyo mtoto wa mwingine, kwa nini mwanangu? Afadhali mngenishambulia mimi kuliko mwanangu wa pekee!”

Hakimu Mkazi Mkuu Viena Amboko alisimamisha ushahidi wa Bi Khamali kwa madai kuwa alihitaji kuwa na utulivu wa kihisia kabla ya kuendelea.

"Ninaelewa kuwa yeye ndiye mama wa mlalamishi ambaye ndiye mjeruhiwa mdogo katika kesi hiyo na amechokozwa hadi kugeuka kihisia alipokuwa akisimulia matukio yanayohusu majeraha ya mtoto wake," aliamua Hakimu Amboko.

“Kwa sababu hiyo ninahisi kwamba tunaahirisha kesi hiyo hadi Septemba 22, 2023 ninapoamini kuwa atakuwa katika hali sawa kutoa upande wake wa hadithi. Upande wa mashtaka unapaswa pia kuwaleta wanafunzi wenzake wa mtoto aliyejeruhiwa kutoa ushahidi.”

Tazama video hiyo ya hisia hapa;