Mshukiwa wa mauaji ya Eric Maigo kuzuiliwa kwa Siku 21

Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 16 alikamatwa siku ya Jumanne katika eneo la Kibra kaunti ya Nairobi.

Muhtasari
  • Katika maombi tofauti, polisi wanasema kwamba mtoto huyo anaaminika ndiye alipanga vurugu zilizosababisha kifo cha Maigo mnamo Septemba 15.

Mshukiwa  anayedaiwa kumuua Mkurugenzi wa Fedha wa Hospitali ya Nairobi hospitalEric Maigo atasalia chini ya ulinzi wa polisi kwa siku 21 ili kuruhusu polisi kukamilisha uchunguzi.

Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 16 alikamatwa siku ya Jumanne katika eneo la Kibra kaunti ya Nairobi.

Katika maombi tofauti, polisi wanasema kwamba mtoto huyo anaaminika ndiye alipanga vurugu zilizosababisha kifo cha Maigo mnamo Septemba 15.

Afisa huyo wa uchunguzi zaidi alisema kuwa mashahidi wakuu bado hawajarekodi taarifa na kuchukua sampuli za DNA kwa uchunguzi wa mkemia wa serikali.

"……afisa mpelelezi bado hajajua majeraha aliyopata wakati akitoroka kutoka eneo la uhalifu, kupeleka faili ya kesi kwa ODPP kwa ajili ya kuchunguzwa na kushauri na sio tu kuwasilishwa kwa walalamikiwa mbele ya mahakama kwa maelekezo zaidi," yasomeka maombi hayo mengine. .

Mtoto huyo, ambaye polisi walisema alikuwa anatoroka, alikamatwa katika kijiji cha Olimpiki huko Kibra, Jumanne usiku.

Alihojiwa na DCI kabla ya kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Muthaiga.

Maigo alipatikana akiwa na majerha 25 ya kuchomwa na visu kulingana na uchunguzi wa maiti.