Mahakama yaahirisha kutoa uamuzi katika kesi ya mauaji dhidi ya Jowie na Maribe

Jaji wa Mahakama Kuu Grace Nzioka alipaswa kutoa uamuzi huo leo, baada ya kumalizika kwa kesi hiyo mwezi Julai.

Muhtasari

• Jaji wa Mahakama Kuu Grace Nzioka alipaswa kutoa uamuzi huo leo, baada ya kumalizika kwa kesi hiyo mwezi Julai, lakini imeripotiwa kwamba hakuweza kufanya hivyo kutokana na ugonjwa.

Jacque Maribe na Jowie Irungu mahakamani
Jacque Maribe na Jowie Irungu mahakamani
Image: MAKTABA

Mahakama kuu jijini Nairobi imeahirisha uamuzi wa kesi ya mauaji dhidi ya Joshua Irungu almaarufu Jowie na aliyekuwa mtangazaji wa televisheni Jacqueline Maribe hadi Desemba 15, 2023.

Jaji wa Mahakama Kuu Grace Nzioka alipaswa kutoa uamuzi huo leo, baada ya kumalizika kwa kesi hiyo mwezi Julai, lakini imeripotiwa kwamba hakuweza kufanya hivyo kutokana na ugonjwa.

Wapenzi hao wawili wa zamani wanashtakiwa kwa mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani ambaye alipatikana amefariki kwa kukatwa koromeo nyumbani kwake Nairobi Septemba 2018.

Joseph Irungu akiwa ameshika bunduki ya kivita akiwa na jeraha la risasi. Mfanyabiashara aliyeuawa Monicah Kimani
Joseph Irungu akiwa ameshika bunduki ya kivita akiwa na jeraha la risasi. Mfanyabiashara aliyeuawa Monicah Kimani
Image: MPASHO

Kesi hiyo ilipomalizika mwezi Julai, upande wa utetezi uliwasilisha hoja zao za mwisho ambapo Irungu na Maribe, kupitia kwa mawakili wao, waliiomba mahakama iwaachilie huru.

Waliteta kuwa upande wa mashtaka ulikosa kuthibitisha bila shaka kuwa wana hatia ya kumuua Monica ambaye alipatikana ameuawa kikatili nyumbani kwake huko Lamuria Gardens.