Mavazi ya Jowie yamhusisha na mauaji ya Monica Kimani

"Matokeo yangu ni kwamba kuna ushahidi dhabiti kuhusu nguo ambazo Jowie alikuwa amevaa katika tarehe halisi."

Muhtasari

• "Upande wa mashtaka ulitoa kaptula ya kahawia na kofia ya rangi ya hudhurungi. Walionyeshwa mashahidi na wakasema zinafanana na kile alichokuwa amevaa," Nzioka alisema.

, mshtakiwa wa kwanza katika mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani, katika Mahakama ya Milimani mnamo Februari 9, 2024. Picha: DOUGLAS OKIDDY
Joseph Irungu Jowie , mshtakiwa wa kwanza katika mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani, katika Mahakama ya Milimani mnamo Februari 9, 2024. Picha: DOUGLAS OKIDDY

Jaji Grace Nzioka amesema kulikuwa na ushahidi wa kutosha kuhusu mavazi ambayo Jowie Irungu alivaa Monica Kimani alipouawa.

Ushahidi unaothibitisha ni ushahidi unaoimarisha au kuthibitisha ushahidi uliopo. Ushahidi kutoka kwa shahidi Pamela unaonyesha kuwa wakati Jowie anaondoka nyumbani, alikuwa amevalia shati jeupe lenye michoro, kofia ya rangi ya hudhurungi na kaptula ya kahawia.

"Upande wa mashtaka ulitoa kaptula ya kahawia na kofia ya rangi ya hudhurungi. Walionyeshwa mashahidi na wakasema zinafanana na kile alichokuwa amevaa," Nzioka alisema.

Jaji Nzioka alisema shahidi huyo aliongeza kuwa Jowie pia aliondoka na begi.Shahidi mwingine pia alithibitisha kile Jowie alikuwa amevaa, kofia ya maroon na kaptula ya kahawia.

"Mashahidi wote wanazungumzia nguo ambazo Jowie alikuwa amevaa, jezi, kaptula ya kahawia na kofia ya maroon," Jaji alisema.

Nzioka alisema bado kofia ya maroon iliibuka kwenye vinywa vya kila shahidi.

"Je, mtuhumiwa anasema si yangu? hakuna ushahidi wa hilo," alisema.

"Matokeo yangu ni kwamba kuna ushahidi dhabiti kuhusu nguo ambazo Jowie alikuwa amevaa katika tarehe halisi."

Mahakama pia imethibitisha kuwa Jowie alimfahamu Monica Kimani kabla ya kifo chake. Jowie ndiye mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya mauaji ya Monica. Alishtakiwa pamoja na Jacque Maribe mnamo mwaka 2018.

Jowie alikuwa amedai kuwa hakumfahamu Monica kabla ya kifo chake.

Hakimu Grace Nzioka alisema suala hilo liliibuka kwa sababu ushahidi wa mshtakiwa wa kwanza ni kwamba hakuwa akimfahamu marehemu kabla ya kifo chake.

"Ni uamuzi wa mahakama hii kwamba ushahidi wa mshtakiwa wa kwanza kwamba hakumjua marehemu kabla ya kifo chake haukubaliki, si wa kweli na ni mawazo ya baadaye na ni ya uongo," Hakimu Grace Nzioka alisema.

IMETAFSIRIWA NA DAVIS OJIAMBO.