Mahakama yatupilia mbali ombo la DPP la kuondoa kesi ya ufisadi ya Tanui

Tanui alikuwa ameshtakiwa kwa malipo yasiyo ya kawaida ya Sh30 milioni kwa usambazaji wa transfoma tatu alipokuwa afisini.

Muhtasari
  • Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Kupambana na Ufisadi Victor Wakumile ameagiza kesi hiyo iendelee hadi tamati.

Ombi la afisi ya DPP kutaka kesi ya ufisadi ya Sh30 milioni inayomkabili aliyekuwa MD wa Kenya Pipeline MD Charles Tanui kuondolewa limekataliwa.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Kupambana na Ufisadi Victor Wakumile ameagiza kesi hiyo iendelee hadi tamati.

Ni shahidi mmoja tu aliyesalia kabla ya kesi kumalizika.

"Mamlaka ya kuondoa kesi sio kamili lakini lazima itumike kwa busara kwa kuzingatia masilahi ya umma," Hakimu alisema.

Tanui alikuwa ameshtakiwa kwa malipo yasiyo ya kawaida ya Sh30 milioni kwa usambazaji wa transfoma tatu alipokuwa afisini.

Alishtakiwa pamoja na Elias Maina ambaye alikuwa meneja mkuu anayesimamia idara ya kiufundi na Josphat Sirima ambaye alikuwa mhandisi mkuu.

Watatu hao walishtakiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi.

Lakini walikanusha mashtaka mbele ya Hakimu Mkuu wa Kupambana na Ufisadi Douglas Ogoti.

Kisha waliachiliwa kwa dhamana ya Sh700,000 kila mmoja au bondi mbadala ya Sh2 milioni na mdhamini mmoja.