DJ Joe Mfalme kuwa shahidi wa serikali katika kesi ya mauaji ya afisa wa polisi

Katika barua hiyo hiyo, DPP alimshtaki mlalamikiwa wa kwanza Allan Ochieng' kwa mauaji hayo.

Muhtasari

• DJ Joe Mfalme sasa atakuwa shahidi wa serikali katika kesi ya mauaji dhidi ya Detective Polisi wa Kabete Felix Kelian.

DJ JOE MFALME akiwa kizimbani na wenzake
DJ JOE MFALME akiwa kizimbani na wenzake
Image: DOUGLAS OKIDDY

Mcheza Santuri DJ Joe Mfalme sasa atakuwa shahidi wa serikali katika kesi ya mauaji dhidi ya Detective Polisi wa Kabete Felix Kelian.

Hii ni baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma katika barua yake ya Aprili 5, 2024, kushauri kuwa watano kati ya saba wawe shahidi katika kesi hiyo.

Katika barua hiyo hiyo, DPP alimshtaki mlalamikiwa wa kwanza Allan Ochieng' kwa mauaji hayo.

Anatarajiwa kushtakiwa katika Mahakama Kuu ya Kiambu Jumatatu, Aprili 8.

Zaidi ya kufuata...