Mahakama yamtaka DPP kupunguza mashtaka ya pasta Mackenzie kutoka 191 hadi 12 pekee!

Mackenzie pamoja na waumini wengine 29 wa kanisa lake wamekuwa kizuizini kwa Zaidi ya mwaka mmoja sasa wakituhumiwa kwa makosa mengi yakiwemo lile la kuwatesa waumini hadi kufa na kuwazika Shakahola.

Muhtasari

• Washtakiwa wote 30 kwa pamoja walikana mashitaka 191 ya mauaji, kinyume na kifungu cha 203 kikisomwa na 204 cha kanuni ya adhabu.

Mackenzie na wenzake.
Mackenzie na wenzake.
Image: ODPP

Mahakama ya juu kaitka kaunti ya Mombasa imemuamrisha ODPP kupunguza mashtaka ya mchungaji mwenye utata Paul Mackenzie kutoka idadi ya 191 hadi 12.

Mackenzie pamoja na waumini wengine 29 wa kanisa lake wamekuwa kizuizini kwa Zaidi ya mwaka mmoja sasa wakituhumiwa kwa makosa mengi yakiwemo lile la kuwatesa waumini hadi kufa na kuwazika katika makaburi ya jumla huko Shakahola.

Jaji Mugure Thande aliamua kwamba idadi ya mashtaka ya mauaji dhidi ya washtakiwa ipunguzwe kutoka 191 ya sasa hadi 12.

 Jaji Mugure, ambaye alitoa uamuzi wake kwa karibu, alibainisha kuwa kupunguza idadi ya mashtaka kutaharakisha haki kwa pande zote na kuokoa muda wa mahakama.

"Hii bila shaka itachukua muda mrefu na itaathiri haki za watuhumiwa katika kesi ya haki," alisema.

Thande alimpa DPP siku 21 kufanya marekebisho ya maelezo yenye makosa ya mauaji kabla ya kuwafungulia mashtaka mapya.

"Ni dhahiri kwamba kuna makubaliano katika kesi hizo mbili ambazo hazipaswi kuwa nyingi. Kwa hivyo ninaelekeza ODPP, ndani ya siku 21, kurekebisha karatasi ya mashtaka ili iwe na makosa yasiyozidi 12," aliamua.

Washtakiwa wote 30 kwa pamoja walikana mashitaka 191 ya mauaji, kinyume na kifungu cha 203 kikisomwa na 204 cha kanuni ya adhabu.

Inadaiwa walitenda makosa hayo katika tarehe isiyojulikana kati ya Januari 2021 na Septemba 2023 katika eneo la Shakahola kaunti ndogo ya Malindi ndani ya Kaunti ya Kilifi.