Afueni kwa Sudi huku akiondolewa kesi ya kughushi vyeti vya masomo

Mahakama imemwachilia huru mbunge wa Kapsaret Oscar Sudi katika kesi ya kughushi vyeti vya masomo.

Muhtasari

•Hakimu Felix Kombo alisema upande wa mashtaka ulishindwa kuanzisha kesi yenye uzito dhidi ya Sudi ili kumpa utetezi.

mbele ya hakimu Felix Kombo katika kitengo cha Kupambana na Ufisadi cha Milimani wakati wa uamuzi wa kesi ambapo alishtakiwa kwa karatasi ghushi za masomo mnamo Juni 7, 2024.
Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi mbele ya hakimu Felix Kombo katika kitengo cha Kupambana na Ufisadi cha Milimani wakati wa uamuzi wa kesi ambapo alishtakiwa kwa karatasi ghushi za masomo mnamo Juni 7, 2024.
Image: DOUGLAS OKIDDY

Mahakama imemwachilia huru mbunge wa Kapsaret Oscar Sudi katika kesi ya kughushi vyeti vya masomo.

Hakimu Felix Kombo alisema upande wa mashtaka ulishindwa kuanzisha kesi yenye uzito dhidi ya Sudi ili kumpa utetezi.

Hakimu alisema kushindwa kutoa na kuthibitisha stakabadhi kunamaanisha kuwa shtaka haliwezi kusimama.

Pia alilaumu vyombo vya uchunguzi kuhusu jinsi walivyopata sehemu ya ushahidi.

Sehemu ya ushahidi ambao ni sehemu ya kesi hiyo ilisemekana kupatikana katika hoteli ambayo hakimu alisema iliibua masuala ya kuaminika.