Shahidi asema Mackenzie alitumia vifungu vya Bibilia kumshawishi

Mackenzie alilenga kushawishi watoto wadogo kuacha elimu

Muhtasari

• Shahidi huyo alikuwa Muislamu mwanzoni kabla ya kuingia dini ya Kikristo kutokana na ushawishi wa babake

• Mackenzie alinukuu vifungu vya Bibilia kuwahadaa watoto wadogo kuacha elimu.

Mackenzie na wenzake.
Mackenzie na wenzake.
Image: ODPP

Shahidi mmoja katika kesi inayoendelea kwenye mahakama ya Mombasa inayohusu mhubiri matata Paul Mackenzie amekiri kuwa Mackenzie aliwashawishi waathiriwa kujiunga naye kupitia vifungu vya bibilia.

Kulingana na shahidi huyo ambaye amewekewa ulinzi, alitoa ushahidi kuwa Mackenzie alitumia vifungu kutoka kitabu kitakatifu cha Bibilia kama vile Mhubiri 12:12, Wakolosai 2:8, Timetheo wa Kwanza 6:20 na Yakobo 3:15.

Mackenzie alilenga kushawishi watoto wadogo kuacha elimu.

Shahidi huyo aliendelea kusema kuwa siku zake katika shamba la Shakahola zilisheheni uwindaji, kulala na kusoma bibilia ila baadaye Mackenzie aliamuru kuwa wakati ulikuwa umefika wa kuongozwa na roho mtakatifu na wala sio Bibilia.

Shahidi huyo alieleza kuwa, "Aprili 2022, baba yangu aliuza vitu vyetu vya nyumbani  ikiwemo televisheni na kitanda na tukafunga safari kwenda kanisani kwa Mackenzie eneo la Furunzi, Malindi. Hapo mmoja wa wafuasi wa kanisa la Mackenzie alitukaribisha na kutupeleka Shakahola ."

Vile vile, shahidi alisema kuwa mama yake mzazi alifunga biashara ya duka la upodozi baada ya Mackenzie kumhubiria dhidi ya wanawake kusuka nywele zao au kutumia bidhaa za urembo.

Awali, shahidi huyo alisema mwanzoni alikuwa Muislamu ila baba mzazi aliyekuwa mfuasi susgu wa Mackenzi,  alimshawishi kuasi dini hiyo na kuwa Mkristo. Hapo ndipo kutokana na mafunzo ya Mackenzie alihasi shule mwaka wa 2020.

Aidha, baada ya kulemewa  kufunga kula, shahidi huyo alijaribu kutoroka madhila ya Mackenzie msituni Shakahola kupitia misitu hadi alipofika sehemu ya Shakahola Madukani alikolala kwa siku tatu. Msamaria mwema alimchukua baadaye na kumpa kazi katika duka la kuuza vita vya ujenzi alikofanya kazi kwa miezi kadhaa.

Kesi hiyo inayohusu Mackenzie na wafuasi wake zaidi ya tisini itaebdelea kuskizwa Alhamisi tarehe 12 mwezi Septemba mwaka 2024