Changamoto za ukosefu wa usalama zinazopatikana North Rift ni matokeo ya uongozi mbaya wa kisiasa-Matiang'i

Muhtasari
  • Pia aliahidi kusaidia IEBC kuzingatia katika kuleta uchaguzi wa kuaminika kwa Wakenya ambao wanatumai kuwachagua Wagombea wanaowapendelea
Waziri wa mambo ya ndani red Matiang'i
Image: Fredrick Omondi

Waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiang'i amewataka Wakenya kuzingatia na kudumisha Amani wakati wa uchaguzi, akisema kuwa serikali pia imeahidi kutoa usalama kwa kutoa mafunzo kwa maafisa zaidi wa polisi na Maafisa wa IEBC ambao watatoa huduma zinazohitajika zitakazowezesha taifa kuendesha zoezi hilo vyema.

Akizungumza wakati wa mahojiano na NTV, Matiang'i anasema kuwa hivi sasa, kuna takriban maafisa 20,000 wa chini ambao wanafunzwa Kiganjo pamoja na Wakuu wengine 300 ambao watasimamia uchaguzi ili kuepusha usumbufu wowote.

Pia aliahidi kusaidia IEBC kuzingatia katika kuleta uchaguzi wa kuaminika kwa Wakenya ambao wanatumai kuwachagua Wagombea wanaowapendelea.

"Sisi kama wizara ya mambo ya ndani tumeamua kufanya kazi yetu ya kuleta usalama wa hali ya juu wakati wa uchaguzi, kwa kuleta maafisa waandamizi wadogo na waandamizi wa Polisi 20,000 na 300 mtawalia ambao sasa wanaendelea na mafunzo huko Kiganjo.

Pia binafsi naahidi kutoa huduma za usalama za kutosha kwa IEBC na kuwa mwezeshaji wa uchaguzi unaoaminika.” Alisema.

Waziri huyo hata hivyo aliongeza kuwa Ameshirikiana na mashirika mengine ya serikali ikiwa ni pamoja na NCIC kujenga mashirika mbalimbali ambayo yanaongozwa na Jaji Mkuu Martha Koome, akisema kuwa ilichukua mafunzo kutoka kwa uchaguzi mkuu wa 2017 na ule wa hapo awali.

"Pia tuna mashirika mengine mengi ambayo yamekuja kushirikiana nasi ikiwa ni pamoja na Tume ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa, na mengine ambayo yanaongozwa na Mhe. Jaji Mkuu Martha Koome, tangu tulipojifunza kutoka kwa chaguzi zilizopita ukiwemo ule wa 2017." aliongeza.

Huku akizungumzia uosefu wa usalama katika eneo la North Rift Matiang'i alisema kuwa;

"Changamoto za ukosefu wa usalama zinazopatikana katika sehemu nyingi za North Rift ni matokeo ya uongozi mbaya sana wa kisiasa ambapo lengo ni kuhimiza watu kupigana..."