Masaibu

‘Alipogundua kwamba sijawahi kuwa na mwanamume mwingine,aliniacha’

‘ Alipogundua kwamba sijawahi kuwa na mwanamume alianza kunichukulia kama mshamba, dhana hiyo yake ilinikwaza sana’ anasema Irene

Muhtasari
  • Lakini utachukuliaje tukio la mwanamme kumkataa mwanamke eti kwa sababu mwanamke huyo ni bikra?
  • Alex  inadaiwa alipogundua kwamba Irene ni bikra alimuambia kwamba hayuko tayari kwa uhusiano  kati yao .

Amesimulia  kisa cha kuhurumisha mwanamke mmoja katika kundi moja la  facebook  ambaye ametoa  sababu  iliyowashangaza wengi kwa kuachwa na mpenzi wake ambaye walikutana naye maajuzi tu kupitia  rafiki wao wa pamoja .  sababu za mtu kuachwa na mpenzi wake huwa nyingi na  nyingine hukubalika .

Lakini utachukuliaje tukio la mwanamme kumkataa mwanamke eti kwa sababu mwanamke huyo ni bikra? Alex  inadaiwa alipogundua kwamba Irene ni bikra alimuambia kwamba hayuko tayari kwa uhusiano  kati yao .

Kulingana naye , hataki kuwa na mtu ambaye hajawahi kufanya mapenzi kwa sababu  ni kibarua kigumu kuanza kumvunja mtu ubikra . Hatua hiyo imempa sana msonono Irene akishindwa  atazungumza na nani kuhusu  masaibu yake ., Amejikuta akijuta kwa nini alihifadhi ubikra wake hadi umri wake wa sasa wa miaka 24 kwani anasema wenzake  wengi wa kike wamekuwa pia wakimfanyia kejeli kwamba bado yeye ni bikra na umri wake mkubwa .

Irene amesema kuanzia shule ya msingi amekuuzwa na maadili ya kidini n ahata shule ya upili hakutaka kufanya mahusiano na wanaume hadi alipomaliza chuo kikuu  kwa sababu anavyofahamu yeye kwa ajili familia yake  ni kumcha mungu sana ,ngono ni kitendo cha kufanywa wakati mtu yupo katika ndoa na amesalia na   ukakamavu wa kujizuia kujiingiza katika majaribio . Ameshangaa  ni vipi uamuzi wake huo unavyoweza kumrudi kwa kumfanya kuachwa na mwanamume ambaye alitarajia angekuwa mume wake . Alex maajuzi amerejea kenya kutoka Canada ambako alikuwa akisomea na  walikuwa wakiwasiliana kwa njia ya mtandao na  Irene kwa takriban miaka mitano.

‘ Alipogundua kwamba sijawahi kuwa na mwanamume alianza kunichukulia kama mshamba, dhana hiyo yake ilinikwaza sana’ anasema Irene

Ameongeza kwamba mpango wake wa hapo awali  ulikuwa kusomea utawa ili awe nun lakini baadaye alibadilisha mawazo yake  baada ya wazazi wake kumshawishi kivingine. Irene sasa anasema anajutia mbona aliacha kusomea utawa kwani hangejipata katika hali hiyo endapo wazazi wake wangemruhusu aendelee na mipango aliokuwa nayo . Anasema wazazi walimfanya kubadilisha mwazo yake kuhusu mkondo huo kwa sababu yeye ndiye mtoto wa pekee .