Mafunzo unapaswa kujifunza katika miaka yako ya 20

Muhtasari
  • Mafunzo unapaswa kujifunza katika miaka yako ya 20
  • Kuna baadhi ambayo hufanya maamuzi katika maisha yao ambayo baadaye huyafurahia lakini wengi wanaishi kujuta

Watu wengi hufanya makosa na kuharibu maisha yao wakitimia miaka yao ya ishirini, huku mwishowe weni wakijuta baadaye.

Kuna baadhi ambayo hufanya maamuzi katika maisha yao ambayo baadaye huyafurahia lakini wengi wanaishi kujuta.

Akina babu zetu waliamini kwamba msichana napaswa kuolewa akiwa na miaka 22-25 ndio muda unaofaa, lakini karnne hii ya sasa hata wanapitisha miaka hiyo na wengi kusema maisha ya kukaa bila mpenzi au bwana na mazuri.

 

Lakini unapaswa kujifunza nini ukiwa katika miaka yako ya mapema ya ishirini?

Haya hapa baadhi ya mafunzo hayo;

1.Mitandao ya kijamii ni ya uongo

Kuna baadhi ya watu wengi ambao hupotoshwa na mitandao ya kijamii wakiwa katika miaka yao ya 20 kwani wanataka kutambulikana na kuiga maisha ya wenzao.

Haya basi habari ndio hiyo mitandao ya kijamii haiwezi kakupeleka mahali fanya uamuzi wako ambao utakusaidia maishani.

2.Mafanikio ya mwenzio hayahusiani na yako

KIla mtu ana maazimio yake na safari ya maisha kila mtu hupita njia tofautii kwa hivyo haupaswi kufanya jambo lolote kwa maana umeona mwezako au rafiki yako amefanikiwa.

 

3.Jipe kipaumbele

Baadhi ya watu wengi hupotea na maisha yao kifilisika baada ya kupa mahitaji ya marafiki zao na familia zao kipaumbele na kujisahau.

Kama wataka usije juta baadaye unapaswa kujipa kipaumbele katika maisha yako.

4.Usiage dunia kwa ajili ya shinikizo

Hapo ndipo vijana wengi hupotea baada ya kupata shinikizo kutoka kwa marafiki zao, na kupotea njia bila ya kujua kwamba ana maisha ya kesho ambayo anapaswa kuishi.

5.Mambo yatakuwa magumu kabla ya kuwe mema

Kuna wale wanataka utajiri wa haraka na hawataki kufanya kazi au kutia bidii katika kazi zao, katika maisha kuna panda shuka ambazo kila mmoja anapaswa kuvumilia.