Jinsi tiba ya saratani ya dhahabu, ubani na manukato inavyohusishwa na Yesu Kristo

Muhtasari

•Majaribio ya kimatibabu yameonyesha kwamba vitu hivi vitatu vinaweza kuwa vya manufaa katika kutibu maumivu kama vile ya mishipa na pumu, na wakati mwingine hata saratani mbaya zinazoua.

Image: GETTY IMAGES

Mapambo yanayotengenezwa katika onyesho la Krismasi huonyesha vitu vitatu vikitolewa kama zawadi. Hadithi inaelezea kuwa wanaume wenye busara walikuja na kumpatia mtoto Yesu dhahabu, ubani na manukato.

Vitu hivi vitatu vina faida nyingine na ndio maana wanasayansi wanavichukulia kama vitu vya thamani.

Majaribio ya kimatibabu yameonyesha kwamba vitu hivi vitatu vinaweza kuwa vya manufaa katika kutibu maumivu kama vile ya mishipa na pumu, na wakati mwingine hata saratani mbaya zinazoua.

Kati ya vitu hivyo, viwili kati yake, manukato na dhahabu vinatumiwa kwa matibabu na mwanasayansi wa Chuo kikuu cha Cardiff nchini Uingereza Dkt. Ahmed Ali ambaye anavifanyia utafiti.

Utafiti kwa ajili ya matibabu ya saratani

Dkt. Ahmed Ali anafanya utafiti kuhusu matumizi ya ubani na dhahabu kama dawa
Dkt. Ahmed Ali anafanya utafiti kuhusu matumizi ya ubani na dhahabu kama dawa
Image: DR AHMED ALI

Vitu vyote hivi hutokana na mti unapooza na unapo nyauka, ubani huwa donge la dhahabu, huku almasi huonekana kama chembe chembe nyekundu na za rangi ya kahawia.

Dkt. Ali, alitoka katika nchi ya Somalia na sasa anaishi Newport, anafahamika duniani kwa utambuzi wa ubani.

Anafanya kazi katika idara ya sayansi ya maisha (bioscience) ya chuo kikuu na hufanya majaribio juu ya jinsi vitu hivi vinavyoweza kutumika kuponya makunyanzi ya mwili pamoja na saratani.

Aligundua kuwa ubani wa Somalia una kemikali tofauti ya ubani wa kawaida na unaweza kutumika kwa tiba nyingi.

Dkt Ali anasema. "Tumegundua kwamba unapotoa chembechembe kutoka katika ubani mbali mbali wa Somalia na kuutumia katika kutibu saratani, unafanya kazi ya kuingia ndani ya utendaji wa mfumo mzima wa seli za saratani kuanzia zilipoanzia hadi zilikosambaa. Hiyo inamaanisha kuwa unaweza kuzuwia kusambaa kwa seli za saratani ," anasema Ali.

Dhahabu pia ina manukato, ambayo pia yanafanyiwa utafitikwa ajili ya matumizi ya tiba ya saratani.

Dkt. katika sayansi ya viumbe hai- Bioscience, Profesa Richard Clarkson, ambaye amekuwa akifanya kazi na Ali katika utafiti , anasema utafiti huo unaweza kufikia mafanikio makubwa katika tiba ya saratani.

"Kwa ujumla, lengo ni kupata vitu vipya na dawa ya kuzuwia kusambaa zaidi kwa seli za saratani mwilini. Hatahivyo, ni vigumu kutekeleza hata katika kliniki ," alisema.

Majaribio ya matibabu kuhusu hili yanachukua muda mrefu, ni ya gharama na magumu, alielezea.

Matumizi mengine ya dhahabu, ubani na manukato ni muhimu

Wanasayansi wanafanya utafiti kubaini iwapo dhahabu, ubani na manukato ya dhahabu vinaweza kutumiwa kama dawa
Wanasayansi wanafanya utafiti kubaini iwapo dhahabu, ubani na manukato ya dhahabu vinaweza kutumiwa kama dawa
Image: GETTY IMAGES

Hatahivyo kulingana na Profesa Clarkson, katika maabara, kitu chochte kinachoharibu seli zenye afya bila kuzidhuru kinachukuliwa kama kitu cha manufaa sana.

" Unapotafuta kitu fulani kinachofanya kazi kwa kung'amua na kuangamiza seli za saratani na sio kudhuru seli zenye afya, chembe chembe za dhahabu zinaweza kuwa za manufaa sana iwapo utazichanganya na ubani ndani yake ," anasema.

"Kihistoria, vitu hivi vimekuwa vikichukuliwa kuwa vyenye manufaa sana, kwa hiyo uchunguzi wake unavutia."

Dkt. Ali anasema wakati alipofanya utafiti faida nyingine ya ubani aliyoibaini ilikuwa ni kuzuwia uvimbe mwilini.

"Ubani pia umebainika kuwa unweza kuwa na manufaa katika kutibu ugonjwa wa arthritis.

Ubani pia umebainika kuwa unaweza hususan kuzuwia dalili maambukizi ya utubo na kuzuwia maradhi ya mfumo wa kutoa haja."

Wanasema kwamba ubani pia una manufaa katika kuzuwia kuoza kwa meno.

Hatahivyo, utafiti wote huu bado uko katika hatua ya mwanzo kabisa, na uko katika kiwango cha maabara, licha ya kwamba vitu hivi vitatu ubani, dhahabu na ubani vimekuwa vikichukuliwa kama vitu vya maana kwa karne nyingi.

Mhadhiri katika masuala ya Historia ya tiba katika Chuo kikuu cha Aberisith, Dkt Rachel Gillibrand anasema alishangaa sana kubaini kuwa vitu hivi vilikuwa vinatumiwa zamani. "Ubani haukutumiwa tu kama manukato, bali ulitumiwa katika kutibu magonjwa mengi ," anasema.

Umuhimu wa kidini wa vitu vyote vitatu

Dhahabu ina historia ya kutibu maumivu ya meno
Dhahabu ina historia ya kutibu maumivu ya meno
Image: GETTY IMAGES

Katika enzi ya Victoria, wakati watoto walipobainika kuwa na minyoo, walikuwa wanapewa mchanganyiko wa ubani na dhahabu na kunyweshwa kama tiba.

Dhahamu ni aina nyingine ya kiungo, lakini imekuwa ikitumika katika dawa.

Dkt. Gillibrand anasema Hippocrates, baba wa tiba ya kisasa, alipendekeza kutumiwa kwa dhahabu kama tiba ya maumivu ya meno miongo kadhaa iliyopita.

Aliongeza kwamba mfupa wa uti wa mgongo wa mwanajeshi Mgiriki uliopatikana wakati ulipofufuliwa ''ulituonyesha dhahiri kwamba wakati ule dhahabu ilitumiwa kwa njia hii, sio tu katika maandishi ."

Dhahabu pia imekuwa ikitumika kutibu saratani

Dhahabu haitumiwi kama kiungo mara nyingi, na chembechembe zake hutumika katika tiba ya kuua seli za saratani (radiation therapy). Hii huifanya mashine ya X-rays kuingia vyema na kuifanya tiba hiyo kuwa yenye ufanisi zaidi.

Hatahivyo, umuhimu ulikuwa tofauti wakati mtoro alipopewa zawadi kwa Kristo maelfu ya miaka iliyopita.

Lakini ubani na dhahabu kwa pamoja vilitumiwa kama manukato, na kwa lengo la zawadi ambayo ilikuwa lazima apewe mtoto Yesu.

Mafuta ya dhahabu yalitumiwa kama nguo ya kujifunika. Dahabu ilichukuliwa kama kitu cha thamani hata wakati ule, kwani ilikuwa na rangi ya kung'aa ambayo ilikuwa na rangi ya mvuto wakati wote.

Askofu wa Right Rev. Gregory Cameron anasema kuwa zawadi hizo tatu pia zina umuhimu wake wa kidini. Hatahivyo, ni nadra kwa Biblia kutaja asili yake.

"Katika Ukristo, Kristo anachukuliwa kuwa na nafasi tatu -Masia, Kasisi na Mfalme ."

"Kwahiyo Manukato yalitolewa kwake kama Masia, Ubani ukatolewa kwake kama Kasisi na dhahabu ikatolewa kwake kama Mfalme."