Kwa nini Kenya ni miongoni mwa nchi zinazoandaa uchaguzi ghali zaidi

Tume huru ya uchaguzi na mipaka[IEBC] imetumia zaidi ya shilingi bilioni 44 katika kura za agosti 9.

Muhtasari

•Kenya ni miongoni mwa mataifa duniani ambazo tume ya uchaguzi zanayogharamika zaidi kufanya kura.

•IEBC imetumia shlingi 2.6B kwa miaka minne iliyopita katika kugharamia shughuli za kesi.

akizungumza katika Bomas of Kenya mnamo Agosti 10, 2022
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati akizungumza katika Bomas of Kenya mnamo Agosti 10, 2022
Image: ENOS TECHE

Kenya ni miongoni mwa mataifa duniani ambazo tume ya uchaguzi zanayogharamika zaidi kufanya kura.

Tume huru ya uchaguzi na mipaka[IEBC] imetumia zaidi ya shilingi bilioni 44 katika kura za agosti 9. Hiki ni kiwango kikubwa cha pesa ambacho kinamgharimu mlipa ushuru.

Kuna gharama zingine kama vile ungarishaji wa mazingira katika vituo kabla na baada ya kura. Haya yanawaathiri wananachi hata kama si moja kwa moja.

Kwanza kufungwa kwa mashule kumechelesha kasi ya masomo.Pia imeongeza matumizi kwa wazazi ambao walilazimika kutafuta nauli kati ya mahitaji mengine ili watoto wao warudi shuleni.

Kama kuna gharama ambayo huwa haiyangaliwi, ni ile ambayo IEBC inatumia kutetea matokeo mahakamani ambapo waliobagwa huwasilisha kesi kutaka matokeo kubatilishwa. Ikiwa kesi zao zitafaulu, tume ya IEBC inahitajika kuandaa upya kura za uchaguzi ingine, hii inawaadhibu walipa ushuru kwa makosa ambayo tume inaweza epuka.

Kesi hazi zinatarajiwa kuongezeka ikilinganishwa na miaka ya awali. Katika mwaka wa 2007, kulikuwa na kesi 388 katika mahakama zote nchini.

Mwaka wa 2013, kesi zilizowasilishwa mahakamani zilikuwa 188 ambazo zilihusisha viti mbalimbali ambavyo vilikuwa vikigombewa.

Kati ya kesi 388 zilizowakilishwa kotini 2007, 174 ilikuwa ya magavana na wawakilishi wadi, 125 ikihusisha wabunge, maseneta na wawakilishi wa wanawake. Katika kategoria hii,kesi kubwa ilikuwa ya wabunge ambapo 98 ya kesi zilitaka ubatilizaji wa matokeo.

IEBC imetumia shlingi 2.6B kwa miaka minne iliyopita katika kugharamia shughuli za kesi.

Kati ya mwaka 2018 na 2021, tume ilitumia asilimia 12.3 ya bajeti yake katika mahakama ya juu ikiwa milioni 859.3 katika mwaka wa 2017/2018.

Huku Raila Odinga wa Azimo la umoja-One Kenya na wengine baada ya kuwasilisha kesi katika mahakama ya upeo, walipa ushuru sasa wanatazamia mabilioni ya pesa kutumika katika shughuli nzima na IEBC kutetea uamuzi wake.

Inakereketa wakenya wakigoma kujishusisha na kura kuu za uchaguzi endapo mahakama itaamrisha IEBC kuandaa upya.Hii itafanyika chini ya siku sitini kwa mujibu wa sheria.

Wakenya walitumia bilioni 10 katika marudio ya uchaguzi wa mwaka 2017 baada ya Jaji David Maraga na wengine kutoa agizo hilo.

Tume itatakiwa kuhakikisha kuwa kuna karatasi za kupiga kura, sanduku za Kiems, kuwaajiri upya maafisa katika vituo zaidi ya 40000, vifaa vingine vya kiteknolojia, usafiri,na usalama.

Ripoti kutoka kwa wizara ya fedha inaoonyesha kwamba billioni 43.9 zilitumika katika marupurupu ya ushuru.