'Tunataka haki,'Daddy Owen avunja kimya baada ya binamu yake kuuawa na polisi

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram Daddy Owen alisema kuwa binamu yake alipigwa risasi ya kichwa.

Muhtasari
  • Kulingana na taarifa hiyo, mwanamume huyo alipigwa risasi baada ya kugombana na polisi huyo, ambaye hatimaye alitiwa mbaroni
Image: INSTAGRAM// DADDY OWEN

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili nchini Kenya Daddy Owen amevunja ukimya baada ya binamu yake kuuawa kwa kupigwa risasi na afisa wa polisi.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram Daddy Owen alisema kuwa binamu yake alipigwa risasi ya kichwa.

Aliendelea kusema kuwa hii ni huzuni na uchungu kwa familia yao.

Alimalizia kwa kusema kuwa wanatafuta haki

"Binamu yangu wa kwanza aliuawa na polisi wakorofi waliompiga risasi kichwani. Hii ni huzuni na uchungu kwa familia yetu. Tunatafuta haki."

Habari za binamu yake kupigwa risasi zilitangazwa na gazetti la Star, huku tukio hilo likiaminika kutokae Jumapili iliyopita, Umoja kaunti ya Nairobi.

Kulingana na taarifa hiyo, mwanamume huyo alipigwa risasi baada ya kugombana na polisi huyo, ambaye hatimaye alitiwa mbaroni.

Aidha msanii Owen hakuweza wazi nini haswa kilitokea ili binamu yake apigwe risasi.

Hizi hapa baadhi ya jumbe za mashabiki a risala za rambi rambi;

evarlistandegwa: My condolences @daddyowen ,it is well.May GOD comfort you and everyone affected 🙏🏾

wairimu1955: Pole Sana mungu ailaze roho yake mahali pema😢😢😢

chris001ke: Pole sana Bro , your family are in my prayers

marion.tammu: So sad! Poleni sana Papa Fololo😢

alindabelle: Woooooiiiiii poleni sana😢😢😢

honalinur: Poleni sana bro