Maswali 5 aliyoyajibu Rais Ruto wakati wa mahojiano

William Ruto aliwaambia wanahabari kwamba Kenya "imefunga breki" katika kukopa tena.

Muhtasari
  • Huduma zote za serikali zitawekwa katika mfumo wa kidijitali katika muda wa miezi sita ijayo, Rais William Ruto amesema
RAIS WILLIAM RUTO
Image: TWITTER

Rais WilliamRuto jana (Jumatano)alifanya mahojiano na vyombo vya habari vya ndani na vya kimataifa kuzungumzia masuala mbali mbali tangu kuchukua hatamu baada ya uchaguzi wa mwaka jana.

Jambo la kwanza kulizungumzia Rais ni uagizaji wa chakula cha GMO,ambapo Ruto alisema na kukiri kwamba hawezi hatarisha maisha ya Wakenya waliomchagua.

Haya hapa baadhi ya mambo 5 aliyoyasema katika mahojiano hayo ya Jumatano usiku;

Ruto uamuzi wa kuagiza vyakula vya GMO

Rais William Ruto ametetea hatua yake ya kuagiza vyakula vilivyobadilishwa vinasaba (GMO).

Ili kuunga mkono hoja yake, Ruto alifichua kwamba vyakula vyote ambavyo nchi imekuwa ikiagiza kwa muda wote vina viambajengo vya GMO lakini alisema viko ndani ya asilimia moja inayohitajika na ofisi ya kukadiria ubora wa bidhaa nchini Kenya (KEBS).

Aliongeza, “Siwezi kuhatarisha maisha ya watu walionichagua...mimi ni mwanasayansi, wanasayansi wote nchini wanakubaliana kwamba GMO haina madhara,” alisema.

Huduma zote za serikali kuwa za kidigitali ifikapo Juni 

Huduma zote za serikali zitawekwa katika mfumo wa kidijitali katika muda wa miezi sita ijayo, Rais William Ruto amesema.

Haya yanajiri huku serikali ikianza njia ya kujenga mapato ya ndani ili kujitegemea

Kenya haitashindwa kulipa deni lake - rais

Rais wa Kenya anasema nchi hiyo haitashindwa kulipa deni lake licha ya changamoto kubwa za kiuchumi.

William Ruto aliwaambia wanahabari kwamba Kenya "imefunga breki" katika kukopa tena.

Ilipofika Septemba mwaka jana, serikali yake ilisema itapunguza ukopaji wa gharama kubwa wa kibiashara kwa ajili ya vyanzo vya bei nafuu kama vile Benki ya Dunia.

Nilimfuta kazi aliyekuwa  mkuu DCI 

Rais wa Kenya William Ruto amefichua kwamba alimfukuza kazi mkuu wa zamani wa DCI kutokana na visa vya watu kutoweka kwa lazima na mauaji ya kiholela.

Rais Ruto alikuwa amesema awali aliyekuwa mkurugenzi wa uchunguzi wa jinai George Kinoti amejiuzulu.