Ramadhani: Fahamu mbinu za kupunguza kiu wakati wa mfungo

Je, ulaji wa iliki na mtindi wakati wa Daku na Iftar hupunguza kiu?

Muhtasari

•Inashauriwa kijumla kunywa maji mengi pamoja na kula viungo kama iliki, majani ya mnanaa na pia mtindi (Yogurt)wakati wa daku .

•Protini ya maziwa kutoka kwa bidhaa za maziwa inakolea ndani ya tumbo kwa muda mrefu na kutokana na hili, hakuna hisia ya njaa kwa muda mrefu.

Image: BBC

Katika mwezi wa Ramadan, iwe ni chakula cha daku au Iftar, kutunza chaguo la kila mtu ndani ya nyumba na kuongeza mapishi mapya kwenye chakula kila siku imekuwa sehemu ya mila.

Kwa mujibu wa kalenda ya Kiislamu, kufunga kwa mwezi wa Ramadhan wakati mwingine huja wakati wa baridi na wakati mwingine katika majira ya joto. Sasa iwe ni kufunga kwa muda mfupi au muda mrefu, swali moja mara nyingi ambalo hua katika ndimi za wengi ni jinsi ya kuzuia kiu.

Mara tu Ramadhan inapoanza , kila mtu huanza kujaribu kila mbinu ya kuzuia kiu wakati wa mwezi huu mtukufu.

Inashauriwa kijumla kunywa maji mengi pamoja na kula viungo kama iliki, majani ya mnanaa na pia mtindi (Yogurt)wakati wa daku .

Inasemekana kwamba ikiwa unatumia vitu hivi katika Daku , basi saumu yako kwa zaidi ya masaa 14 itapita kwa raha bila kiu.

Maziwa yaliyoganda
Image: BBC

Je mtindi unaweza kukata kiu ?

Lakini kuna ukweli kiasi gani katika mambo haya, na je, njia hizi kweli zinasaidia kupunguza kiu ya kila siku?

Tulizungumza na Zainab Ghayur, mtaalam wa upishi katika Hospitali ya Kimataifa ya Shifa ya Islamabad, sio tu juu ya vidokezo hivyo, lakini pia juu ya nini cha kula kwa gharama ya chini katika nyakati hizi za mfumuko wa bei na nini ambacho hakitahitajika .

Kijumla Kitambaa cha (dastarkhwan) ambacho hutandikwa juu ya meza ya maandalizi ya chakula kinatambulika kuwa na umuhimu mkubwa katika mila na desturi za jamii za Waisilamu barani Asia .

Ikiwa tunazungumzia wakati wa Daku , basi kuna orodha ndefu ya vyakula vingi kama vile mayai, salans , nyama , mtindi, nyama, maziwa yaliogandishwa ambayo hutumiwa kila siku.

Kulingana na mtaalam wa chakula Zainab Ghayur, sio lazima chakula chenyewe kiwe kiko kwenye orodha ya lishe bora , kwa kawaida hakichukuliwi kuwa Daku na Iftar. Kulingana na yeye, ni muhimu kuingiza vitu na vyakula vya jadi ambavyo husaidia kurejesha nguvu siku nzima, huku akisisitiza kuwa maziwa ya mtindi au Yogurt iko katika orodha ya juu

"Matumizi ya mtindi wakati wa Daku ni kitu kinachohimizwa sana. Protini ya maziwa kutoka kwa bidhaa za maziwa inakolea ndani ya tumbo kwa muda mrefu na kutokana na hili, hakuna hisia ya njaa kwa muda mrefu.

Kulingana naye, "Yogurt ina viambato vingine ambavyo pia husaidia katika kutimiza hamu yako ya maji kwa sababu ina madini ya Pottasium na nazo kemikali za sodium ni kidogo."

Dk. Zainab anasema kuwa baadhi ya watu hujumuisha sukari au vitu vingine kwenye (Yogurt)mtindi, wasipojumuisha, basi mtindi bado unasaidia katika kukidhi mahitaji ya kuongeza nguvu wakati wa Daku .

Kwa swali la iwapo majani mabichi ya iliki na mnanaa(Mint) hupunguza kiu katika hali ya kufunga, alisema, "Hakuna tatizo kutafuna iliki ya kijani na majani ya mint kwenye saladi au vivyo hivyo kwa sababu vitu hivi vyote viwili huwa vinaleta utofauti mwilini lakini havihusiani moja kwa moja." ili kupunguza kiu yako."

Chakula cha Iftar
Image: BBC

Chai au kahawa haipaswi kuwa chungu sana'

Chai
Image: BBC

Zainab Ghayur anasema kwamba kumejumuishwa mambo mengi yasiyo ya lazima kiutamaduni katika mlo wa Ramadhani. Kulingana na yeye, ni bora kula chakula sawa wakati wa Iftar ambacho huwa tunakula kwa kifungua kinywa au Daku .

Anasema kwamba kwa watu wanapaswa kukaa tumbo tupu kwa saa nyingi katika hali ya kufunga, kwa hio lazima watu wakumbuke baadhi ya mambo katika mlo. Anasema "Tunapojaribu kupunguza kiu, tunapaswa kula angalau vitu ambavyo vina chumvi ."

Kulingana na mtaalamu wa lishe Zainab Ghayur, ikiwa tunakula chakula aina ya paratha kwa kiamsha kinywa, basi kula paratha wakati wa Daku huongeza hatari ya kiungulia au asidi wakati wa mchana. Badala yake chukua mayai na chapati,samaki aina ya salmon pia inaweza kuliwa. Hakuna tatizo katika hilo.

Kulingana naye, kachumbari hazipaswi kuliwa kabisa wakati wa daku kwa sababu kachumbari ina chumvi nyingi. Kadiri tunavyokula vyakula vyenye chumvi nyingi katika wakati wa Daku , ndivyo kiu inavyoongezeka mchana na tunaweza kuwa wahanga wa uhaba wa maji.

Pia ameshauri kwamba “Ikiwa utakunywa chai au kahawa wakati wa daku , jaribu isiwe chungu sana lakini itengenezwe na maziwa zaidi kwa sababu kiasi kikubwa cha usugu wa majani au kafeini utaondoa maji mwilini haraka na unaweza kuhisi kiu