Magonjwa yanayoweza kusambazwa na wanyama wafugwao nyumbani, vidokezo vya kuyaepuka

Kuna zaidi ya magonjwa 200 yanayohusishwa.

Muhtasari

•Kuishi na wanyama mfano mbwa, paka, sungura, mbuzi, ng'ombe au mnyama mwingine yoyote kuna faida kwa afya na husaidia ustawi. 

•Ikiwa imegunduliwa kuwepo kwa tatizo hili kwa paka, matibabu yake ni kuiondoa kutoka kwa mwili wa paka husika.

Image: BBC

Ni jambo lisilopingika kuwa wanyama tunaowapenda kuwafuga nyumbani wamekuwa sehemu muhimu ya familia nyingi na wanapata nafasi zaidi na zaidi (na kupendwa) kutoka kwa wanaowafuga (binadamu).

Kuishi na wanyama mfano mbwa, paka, sungura, mbuzi, ng'ombe au mnyama mwingine yoyote kuna faida kwa afya na husaidia ustawi. Lakini utunzaji wa wanyama hawa lazima uchukuliwe kwa umakini ili ukaribu wao na binadamu usidhuru afya zetu: wanyama wanaweza kuambukiza magonjwa mengi, baadhi yao yanaweza kuwa mabaya na kuleta madhara zaidi, kama vile kichaa cha mbwa na toxoplasmosis.

Kuna zaidi ya magonjwa 200 yanayohusishwa hapa. Lakini magonjwa 6 kati ya 10 ya kuambukiza ambayo huathiri watu husambazwa na wanyama, ikiwa ni pamoja na wanyama tunaowafuga nyumbani, kwa mujibu wa Kituo cha Marekani vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC).

Lakini hili lisiwe sababu ya kuachana na mawazo ya kuwa na mnyama au wanyama nyumbani au kuachana na mnyama ambaye tayari ni sehemu ya maisha ya familia yako.

1. Kutana mara kwa mara na daktari wa mifugo

Image: BBC

Hata kama mnyama wako unayemfuga yuko sawa, lazima ufanye tathmini ya mifugo yako angalau mara moja kwa mwaka.

Wakati wa mashauriano, baadhi ya vipimo vya msingi vinaweza kufanyika na utaulizwa maswali kuhusu afya ya mnyama.

Hii pia ni fursa nzuri ya kufanya mambo mawili ambayo ni ya msingi kwa afya ya mnyama. Ya kwanza ni kuhusu rekodi ya chanjo (kuna dozi ambazo lazima wanyama wapatiwe kila mwaka).

2. Fanya usafi na chukua tahadhari maalum

Image: BBC

Ukizungumzia usafi, jambo lingine muhimu ni utunzaji wa vyombo ambapo chakula na maji ya mnyama huwekwa, pamoja na mahali ambapo mnyama hujisaidia kinyesi.

Mbali na minyoo, hali hii inaweza kuwa chanzo cha bakteria.

Moja ya wasiwasi zaidi, hasa tunapozungumzia paka, kuna kitu kinaitwa Toxoplasma gondii, ambacho husababisha ugonjwa unaojulikana kama toxoplasmosis.

Wakati mwingine toxoplasmosis inaweza kuleta madhara mabaya sana. Inatia wasiwasi hasa kwa wanawake wajawazito, kwani inaweza kusababisha kuharibika kwa mimba.

Ili kuepuka hatari hii, kile ambacho wataalam wanapendekeza ni kufanya uchambuzi wa kinyesi ambao unatathmini uwepo wa Toxoplasma gondii kwa paka.

Majaribio yanaonyesha hili kwa watoto wa mbwa, ambao hubeba bakteria hii mara nyingi zaidi.

Ikiwa imegunduliwa kuwepo kwa tatizo hili kwa paka, matibabu yake ni kuiondoa kutoka kwa mwili wa paka husika.

3. Tunza mazingira

Image: BBC

Mahali ambapo vitu vya mnyama unayemfuga vinatunzwa ni sehemu nyingine muhimukuizingatia ili kuepuka bakteria na vimelea vingine vinavyosababisha maambukizo.

Kwa Ulaya wanakuwa na sanduku la takataka la paka au kitanda cha choo cha mbwa, kwa mfano, lakini kwa waafrika wengi wanakuwa na mabanda ya mbwa ama wanawaachia tu, muhimu, vitu vya wanyama wako vikawekwa mbali na jikoni.

Wanyama wanaojisaidia hovyo wanaweza kupewa mafunzo.

vinyeji vyao vinapaswa kuondolewa haraka iwezekanavyo, na eneo lenye uchafu linapaswa kusafishwa kwa sababu linaweza kuwa sehemu ya kusambaza bakteria.

4. Jihadharini na anga ya nje

Image: BBC

Pia unapaswa kuzingatia mazingira ya nje ya nyumba.

Silva, ambaye pia ni mshauri wa zoonoses kwa Wizara ya Afya, anaonyesha kuwa maeneo haya mara nyingi ni mahali pa mawasiliano kati ya wanyama wafugwao na wanyama pori.

Kuna hatari kutoka kwa popo wanaokuja mjini "au kugusa mkojo wa panya," anaeleza daktari na profesa katika Shule ya Tiba ya Chuo Kikuu cha Kipapa cha Kikatoliki cha São Paulo (PUC-SP).

Mkojo wa panya unaweza kuwa na bakteria ya Leptospira, ambayo husababisha leptospirosis.

5. Kumtoa uwezo wa kuzaa mnyama wako'

Utaratibu huu ni rahisi, salama na huzuia mnyama kuwa na watoto wasiotarajiwa. Lakini Silva anaelekeza kwenye faida nyingine ya kutozaa: Baadhi ya spishi, kama vile paka, huwa na vurumai wakati wa msimu wa kuzaliana.

Katika makabiliano haya kuna kuumana na mikwaruzo hutokea. Majeraha haya ni vyanzo vya maambukizi ya virusi, bakteria, fangasi na magonjwa mengine.

Kwa paka aliyehasiwa hawezi kujiingiza kwenye makabiliano haya kwa kuwa hana uwezo wa kuzaa na hilo linasadia kupunguza uwezekano wa kusambaa kwa mahonjwa.