FAIDA ZA KONOKONO

Fahamu faida maalum za nyama ya konokono

Inaaminiwa kuwa nyama yake huwa na lishe bora, pia ni tiba ya ugonjwa wa moyo

Muhtasari

• Konokono huwa na wingi wa protini. Weupe waio na nyama au wasio na mifupa wanaweza kupikwa kwa mafuta au hata kuchomwa. Huwa na vitamini B,D na E.

•Unapoanza maandilizi ya kufanya biashara ya kuuza konokono au kutumia kama chakula, unafaa uchukue tahadhari kubwa hasa kubaini konokono sawa, au wenye sumu.

 

Konokono kutumika kutengeneza dawa ya kikohozi
Konokono kutumika kutengeneza dawa ya kikohozi
Image: BBC NEWS

Konokono, kuna ukweli uliofichika ndani ya wanyama hawa wanaojulikana kwa mwendo pole kando na kinyonga na  kobe.

Konokono, wanajulikana kuwa na mazuri chungu nzima japokuwa binadamu wengi huwachukia wanyama hawa. Kulingana na utafiti wa wanasayansi wanaoangazia lishe bora, wameorodhesha konokono kuwa miongoni mwa wanyama wenye manufaa mwilini mbali na kuwa na tiba ya kitamaduni.

Katika taifa la Kidemokrasia ya Kongo, wakulima nchini humo wanafanya biashara ya konokono kama ya wanyama wengine wale. Wakati kuna mvua kubwa, wanyama hao hutokea na ambapo wakulima huwakusanya kisha kuwapeleka mijini ambapo huwauza wakiwa hai au wakiwa wamekaushwa.

Wafikapo katika vituo wanakodhamiria kuwauza, wanyama hao huuzwa tena, na rundo la moluska 3 au 4 zikileta hadi faranga za Kongo elfu mbili au 0.86 USD baada ya ununuzi wa awali wa 1500 faranga ya Kongo au 0.65 USD.

Celestine amekuwa mfanya biashara wa konokono kwa zaidi ya miaka 10, na ambapo ameeleza katika mitandao yake ya kijamii uzuri wa mafunaa ya biashara hiyo.

“Kwa biashara hii pekee, ninaweza kusomesha watoto na wajukuu, kulisha familia yangu na kwa sasa kujenga nyumba,” alieleza.

Katika eneo la Jangwa la Sahara, Afrika Kusini, konokono ni mojawapo ya wanyama wanaoliwa sana ambapo eneo la bonde la Mto Kongo wanyama hao hutafutwa kwa ajili ya nyama yao na ambayo ina lishe bora.

Ukusanyaji wa wanyama hawa hujaanza leo, maana pia biashara hiyo inaendelezwa na watu katika eneo la Pwani ambapo magamba ya baadhi ya konokono hukusanywa na kisha kwenda kuunda mapambo au vifaa mbalimbali.

Kulingana na tafiti za Kisayansi, Konokono huwa na wingi wa protini. Weupe walio na nyama au wasio na mifupa wanaweza kupikwa kwa mafuta au hata kuchomwa. Huwa na vitamini B,D na E. Huwa na utendaji mzuri wa mfumo wa moyo na mishipa.Nyama hiyo inaweza kuliwa pamoja na wali, ndizi, mihogo na vyakula vingine.

Gamba la konokono pia hutumika kwa kinga za mwili ambapo huchomwa na kisha kusagwa. Majivu yake huchanganywa na mimea kadhaa au mafuta ya wanyama ili kutibu maumivu ya kichwa kwa watoto na majeraha.

Kitamaduni, gamba hilo pia linaaminika kutumika kuzuia ajali pamoja na magonjwa. Kuliweka gamba hilo ndani ya nyumba, iliaminiwa kuwaepusha watu dhidi ya waoweza kuwa wavamizi au wezi.

Konokono ni wa aina nyingi, ambapo kuna zaidi ya aina 500 za konokono na wote wakiwa na manufaa yao. Wengi wao wana sumu, hasa wenye chembechembe nyekundu za damu mwilini, ambazo hujulikana kama koni.

Unapoanza maandilizi ya kufanya biashara ya kuuza konokono au kutumia kama chakula, unafaa uchukue tahadhari kubwa hasa kubaini konokono sawa au wenye sumu. Inashauriwa, kushauriana na wataalam wa wanyama hao, ili kuupata ushauri mwafaka.