Vitendo vinavyoweza kujeruhi nyeti ya mwanamume wakati wa mapenzi - Ripoti

Mbinu za kujamiiana kama vile mwanamke kukalia uume inatajwa kuwa chanzo kikuu cha ajali za kuvunjika uume.

Muhtasari

• Kwa mujibu wa  ripoti ya utafiti huo, ajali ya kuvunjika uume si suala lenye kujitokeza mara kwa mara, kesi hizi kuripotiwa  mara 1 kati ya wanaume 175,000.

 

Kuvunjika kwa uume kunaweza kutokea kwa sababu ya kubadilisha mitindo ya kujamiana wakati wa kushiriki tendo la ndoa.
Kuvunjika kwa uume kunaweza kutokea kwa sababu ya kubadilisha mitindo ya kujamiana wakati wa kushiriki tendo la ndoa.
Image: BBC NEWS

Madaktari nchini Tanzania wamegundua kuwa mbinu ya kujamiana inaweza kufanya uume  kuvunjika.

Kwa mujibu wa tovuti ya BONGO5, Utafiti huo wa madaktari wa idara ya Magonjwa ya Mfumo wa Mkojo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, Tanzania imebainisha kuwa mbinu ya kushiriki ngono inaweza kusababisha uume uliyosimama kwa muda mrefu kuvunjika.

Utafiti wa madaktari hao umechapishwa kwenye Jarida la kimataifa la Upasuaji (International Journal of Surgery Case Reports, 108(2023)108415) wameripoti kufanya upasuaji wa kuunganisha uume wa mvulana mwenye umri wa miaka 27 uliyovunjika wakati akijamiana na mpenzi wake.

Kwa mujibu wa taarifa ya utafiti huo, ajali ya kuvunjika uume si suala lenye kujitokeza mara kwa mara, kesi hizi kuripotiwa  mara 1 kati ya wanaume 175,000.

Hata hivyo, utafiti huo unadokeza kuwa, tafiti zilizofanyika katika mataifa ya Ulaya na Marekani zimeonyesha kuwa asilimia 93.3 ya ajali za uume hutokana na kujamiana, ambacho kilikuwa chanzo cha ajali ya Uume aliyopata kijana aliyetibiwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa.

Vile vile, ajali za kuvunjika uume kwa kujichua zilifuata kwa ukaribu katika nafasi ya pili kwa  asilimia 10.

Mitindo ya kujamiiana kama vile Mwanamke kukalia uume inatajwa kuwa chanzo kikuu cha ajali za kuvunjika uume. Imeeleza taarifa hiyo.