Kenya inaongoza katika orodha ya nchi karimu zaidi katika kanda ya Afrika

•Katika orodha ya nchi karimu zaidi Afrika, Kenya inaongoza huku iikishikilia nafasi ya tatu duniani ikifuatwa na Liberia na Nigeria.

Muhtasari

•Katika ya nchi ambazo raia wao wako tayari kuwasaidia wageni, Jamaica inaongoza ikifuatwa na Liberia, Libya, Nigeria, Kuwait, Senegal, Kenya, Marekani na Sierra Leonne.

•Indonesia ndilo taifa ambalo linakisiwa kuwa watu wakarimu zaidi duniani, wakati inapokuja suala la kutoa na kuchangia Misaada. 

Image: BBC

Watu katika baadhi ya nchi maskini zaidi na zenye matatizo duniani wameonekana kuwa watu wa kutoa misaada zaidi.

Wakfu wa World Giving Index imesema Raia wa Indonesia,Ukraine na Kenya wana uwezekano mkubwa wa kuchangia misaada, kusaidia mgeni au kujitolea kwa wakati wao.

Raia wa Uingereza ni miongoni mwa wanaochangia fedha nyingi zaidi lakini hawakotayari kusaidia watu ambao hawafahamu.

Indonesia ndilo taifa ambalo linakisiwa kuwa watu wakarimu zaidi duniani, wakati inapokuja suala la kutoa na kuchangia Misaada. Hii ni kwa mujibu wa wakfu wa kutoa misaada ya kibinadam wa he Charities Aid Foundation (CAF).

Ripoti hiyo ya CAF inayoratibu mpango wa uchangishaji kwa ajili ya misaada, ni moja ya utafiti wa kina uliowahi kutolewa, huku mamilioni ya watu wakihojiwa kote duniani tangu mwaka wa 2009.

Uchunguzi wa mwaka huu ulikusanya maoni kutoka kwa nchi mia moja arubaini na mbili duniani ambako watu waliuzwa maswali matatu.

La kwanza ikiwa je umewahi kumsaidia mgeni? umewahi kumpa fedha mgeni na swali la tatu ni je umewahi kujitolea kumsaidia mgeni katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita?

Licha ya kuwa raia wa taifa la Uingereza ndio wanaochangia zaidi, harakati za kutoa misaada hasa fedha, taifa hilo limeshuka hadi nafasi ya hamsini na nane katika orodha ya mataifa ambayo raia wake wanajitolea kwa kazi za hiari na pia kushuka hadi nafasi ya 112 katika orodho ya nchi ambazo raia wake wanaweza kumsaidia mgeni.

Mataifa yaliyopanda tena hadi nafasi kumi bora

Katika orodha ya nchi karimu zaidi katika kanda ya afrika, Kenya inaongoza huku iikishikilia nafasi ya tatu duniani ikifuatwa na Liberia na Nigeria.

Katika orodha ya nchi zinazochangia fedha zaidi harakati za kutoa misaada duniani, Myanmar inashika nafasi ya kwanza, ikifuatwa na Indonesia, Uingereza, Ukraine na Malta.

Katika ya nchi ambazo raia wao wako tayari kuwasaidia wageni, Jamaica inaongoza ikifuatwa na Liberia, Libya, Nigeria, Kuwait, Senegal, Kenya, Marekani na Sierra Leonne.

Na katika orodha ya nchi ambazo raia wake wako tayari kujitolea muda wao Liberia inashika nafasi ya kwanza duniani ikifuatwa na Indonesia, Tajikistan, Kenya na Sri Lanka.

Marekani imeshika nafasi tanO mwaka huu, Canada ya nane, New Zealand nayo ikiwa katika nafasi ya kumi.

Neil Heslop ambaye ni afisa mkuu mtendaji wa wakfu huo wa kutoa misaada wa Charities Aid amesema kuwa ripoti ya mwaka huu imetoa taswira tofauti katika nchi mbali mbali hasa Uingereza.

Ameongeza Uingereza imesalia kuwa nchi karimu zaidi duniani kwa kuchangia hazina mbali mbali za kutoa misaada hata hali ikiwa ngumu.

Amesema kutoa au kuchangia wakati wa dhiki ni njia moja ya kujenga mahusiano kati ya jamii mbali mbali kote duniani na kwamba kuna haja ya jamii zote kushirikiana.

Tunahitaji kila mara kukuza utamaduni wa kutoa ili kutuleta sote pamoja na kupata pesa zaidi kutiririka ili kusaidia jamii zenye shida kote duniani.

Ameongeza kuwa ni jukumu letu sote, lakini serikali inaweza kuchukua uongozi kwa kuandaa mkakati wa kitaifa wa na utoaji wa hisani.