Faida za wanandoa kulala vitanda viwili tofauti

Kuna faida nne kuu za wanandoa kulala katika vitanda tofauti.

Muhtasari

•Utafiti unaonyesha ikiwa wanandoa wanalala vitanda viwili tofauti au vyumba viwili - kuna faida za kiakili na kimwili.

•Wanandoa kulala katika vitanda viwili tofauti au vyumba viwili tofauti kunaweza kupunguza mabishano.

Image: BBC

Ni kawaida kwa wanandoa kulala vitanda tofauti nyakati fulani, mmoja wenu anaposafiri au kuugua.

Utafiti uliochapishwa katika mtandao wa relationshipsnsw.org.au -unaonyesha ikiwa wanandoa wanalala vitanda viwili tofauti au vyumba viwili - kuna faida za kiakili na kimwili.

Kuna faida nne za wanandoa kulala katika vitanda tofauti.

Usingizi mzuri

Image: BBC

Wanandoa kulala vitanda tofauti kunaweza kuboresha usingizi wao. Kulala kitanda kimoja kunaweza kuleta changamoto na usumbufu, ikiwa mpenzi wako anakoroma sana - lakini kulala peke yako unapata usingizi mzuri na kupumzika vizuri zaidi.

Na hii ni habari njema, kwa sababu usingizi usiokatishw katishwa ni muhimu kwa afya jumla ya mtu.

Ukosefu wa usingizi huongeza hatari ya kupata matatizo ya kiafya, ikiwa ni pamoja na unene, ugonjwa wa kisukari na ugonjwa wa moyo, kulingana na Harvard Medical School.

Mabishano ya Wanandoa

Image: BBC

Wanandoa kulala katika vitanda viwili tofauti au vyumba viwili tofauti kunaweza kupunguza mabishano.

Wanandoa wengi hukutana baada ya siku ndefu ya kazi na kuchoka. Lakini ikiwa umekuwa na siku mbaya au umechoka na huko tayari kuzungumza na mpenzi wako, kulala kitanda au chumba tofauti kutaepusha mabishano.

Nafasi zaidi

Image: BBC

Baadhi ya watu hupenda kulala peke yao na kujitandaza kitandani lakini wanapokuwa na wenzi wao hujihisi kubanwa na kukosa raha, hivyo huhitaji kuwa na nafasi ya kutosha kitandani.

Kwa maneno mengine, wanataka nafasi ambayo itawawezesha kujifurahisha na kujitanafasi.

Usumbufu wa Asubuhi

Image: BBC

Wanandoa wengi huwa na ratiba tofauti za kazi. Huamka asubuhi mapema na kumsumbua mwenza wake ambaye bado amelala.

Kwa hiyo ikiwa wana ndoa wanalala katika vyumba viwili tofauti, wataepuka usumbufu wa namna hii.

Zingatia haya kabla ya kufanya maamuzi

Wanandoa wanapaswa kuzingatia mambo haya kabla ya kuamua kulala vitanda au vyumba viwili tofauti:

Ikiwa usingizi wako unaathiriwa na kulala kitanda kimoja na mpenzi wako. Ikiwa mnagombana mara kwa mara ama ikiwa mmoja anakoroma sana.