Wanaume wanaotumia Viagra wanaweza kupunguza hatari ya kupoteza kumbukumbu - utafiti

Dawa mbili mpya za Alzeimer's zimeonyesha uwezo kubwa katika kupunguza kasi ya ugonjwa wa kupoteza uwezo wa kukumbuka.

Muhtasari

•Katika utafiti uliowahusisha wanaume zaidi ya 260,000, wanaotumia dawa hiyo walikuwa na uwezekano mdogo wa 18% kupata hali inayosababisha matatizo ya kiakili ya kupoteza uwezo wa kukumbuka.

Image: BBC

Wanaume wanaotumia madawa ya matatizo ya nguvu za kiume, kama vile Viagra, wanaweza kupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa ubongo wa Alzeima, utafiti umebaini.

Katika utafiti uliowahusisha wanaume zaidi ya 260,000, wale ambao wanatumia dawa hiyo walikuwa na uwezekano mdogo wa 18% kupata hali inayosababisha matatizo ya kiakili ya kupoteza uwezo wa kukumbuka , kufikiria au kufanya maamuzi yanayovuruga shughuli zao za kila siku (hali ya kiafya inayofahamika kama dementia)

Lakini utafiti zaidi unahitajika ili kuthibitisha kwamba madawa ya kuongeza nguvu za kiume yanasababisha athari katika utendaji wa moyo.

Dawa mbili mpya za Alzeimer's zimeonyesha uwezo kubwa katika kupunguza kasi ya ugonjwa huo katika hatua zake za awali.

Kwa kushambulia ute unaonata unaoitwa beta amyloid ambao hujilimbikiza juu ya ubongo wa watu wenye Alzheimer's, dawa hiyo inaweza kubadilisha jinsi ugonjwa huo unavyotibiwa .

Lakini wanasayansi pia wanaendelea kutafuta dawa zilizopo ambazo zinaweza kuzuia au kuchelewesha kutokea kwake.

Rekodi za maagizo

Dawa kama vile Viagra hapo awali zilitengenezwa kwa ajili ya kutibu shinikizo la damu na hali ya kupungua kwa mtiririko wa damu kwenye moyo (angina). Hufanya kazi kwa kutendea kazi kama mjumbe anayetuma ujumbe wa seli na pia kuweza kuunganishwa na kumbukumbu.

Pia zinajulikana kuathiri shughuli za seli za ubongo, na utafiti katika wanyama unapendekeza kuwa zina athari ya kinga kwenye ubongo.

Katika utafiti huo mpya wa ubongo, watafiti kutoka Chuo Kikuu cha London College waliangalia rekodi za maagizo ya maelfu ya wanaume wenye matatizo ya nguvu za kiume, wakilinganisha wale waliopewa dawa hizo na wale ambao hawakupewa.

Katika kipindi cha miaka mitano iliyofuata, walipata visa 8.1 vya Alzeimer's kwa kila mtu miongoni mwa watu 10,000 katika kundi lililopewa dawa hizo, na visa 9.7 katika kundi ambalo halikuzitumia.

Wanaume ambao walikuwa wamepewa maagizo mengi zaidi ya dawa za kutibu tatizo la kukosa nguvu za kiume walikuwa na uwezekano mdogo wa kupata Alzheimer's, na hilo lilionyesha kuwa matumizi ya mara kwa mara ya dawa hiyo yanaweza kuwa na athari kubwa kwa ugonjwa huo.

Watafiti wanasema utafiti wao hauonyeshi kuwa dawa zenyewe zilikuwa zinapunguza hatari ya watu ya kupata Alzheimer's, lakini zinaweza kuashiria njia mpya ya utafiti.

Mwandishi mkuu wa utafiti huu Dkt Ruth Brauer alisema: "Utafiti zaidi unahitajika ili kuthibitisha matokeo haya, kujifunza zaidi kuhusu faida na njia zinazowezekana za dawa hizi na kuangalia kipimo bora zaidi."

Watafiti pia wanataka kufanya majaribio kwa wanawake na wanaume, ili kuona ikiwa dawa hiyo ina athari yoyote.

Kuna sababu nyingi ambazo zinaweza kusababisha ugonjwa huo. Utafiti huo ulirekebisha matokeo yake kwa baadhi yao, ikiwa ni pamoja na umri, hali za kiafya, dawa nyingine zilizotumiwa na ikiwa mshiriki alikuwa mvutaji sigara.

"Utafiti huu hauthibitishi kwa uthabiti kwamba dawa za ukosefu wa nguvu za kiume hupunguza hatari ya Alzheimer's, lakini unatoa ushahidi mzuri kwamba aina hii ya dawa inafaa kuchunguzwa zaidi katika siku zijazo," anasema Profesa Tara Spires-Jones, kutoka Chuo Kikuu cha Edinburgh, na rais wa Uingereza sayansi ya ubongo.

Dkt Francesco Tamagnini, mtaalamu wa magonjwa ya neva katika Chuo Kikuu cha Reading, anasema ulikuwa "utafiti mkubwa", lakini ushahidi mgumu zaidi kuhusu jinsi dawa hiyo ilivyoathiri ubongo ulihitajika.

"Inaweza kuwa inatoa athari ya matibabu inayoathiri moja kwa moja (ikiwa dawa inaweza kuvuka kizuizi cha ubongo wa damu) na / au kwa kuongeza mtiririko wa damu, lakini dhana hizi zote mbili zinahitaji kupimwa," alisema.