Fahamu kwa nini hatuhisi kama dunia inazunguka kwa kasi ya maelfu ya kilomita kwa saa

Dunia inaposogea kwa kasi isiyobadilika, tunahisi kana kwamba haisafiri katika anga.

Muhtasari

•Kila kitu duniani, ikiwa ni pamoja na wanadamu, husafiri kwa kasi hii ya mara kwa mara, tunazunguka na sayari, ila hatuhisi safari hiyo.

•Sababu nyingine kuhusu ni kwa nini hatuwezi kutambua harakati za Dunia ni kwamba tumeizoea tu.

Image: BBC

Dunia ni chombo cha anga ambacho hutupeleka kwenye safari ya haraka kupitia anga. Sayari hii nainazunguka kwa kasi ya kilomita 107,280 kwa saa kuzunguka Jua.

Inazunguka kwenye mhimili wake kwa takriban kilomita 1,666 kwa saa kwenye ikweta.

Kwa hivyo ni kwa nini hatuhisi kama tunazungushwa kwa kasi na mpira huu wa anga?

Uthabiti na inertia

Ili kuelewa jambo hili, mwanasayansi wa anga wa Chile Javiera Rey anatupa mfano.

"Fikiria unasafiri kwenye ndege," anasema Javiera Rey, mwanzilishi mwenza wa Star Tres, mpango unaolenga kueneza ujuzi wa kisayansi katika Amerika ya Kusini.

"Unapoondoka, unahisi kama unazama kwenye kiti, na unapotua, unahisi kama unasonga mbele. Hii ni kwa sababu hali hii inamaanisha kwamba huwa tunakaa katika nafasi yetu ya kupumzika."

Image: BBC

Maelezo ya picha, Wakati ndege inapofikia kasi isiyobadilika, Tunahisi kama imesimama tuli.

"Ndege inapofikia ukomo wa kasi ya kusafiri, hautambui kuwa unasonga, unaweza kusimama na kutembea."

Kwa hiyo ndege inaposafiri katika mwendo wa kasi usiobadilika, tunahisi kama imesimama tuli.

Vivyo hivyo kwa Dunia: inaposogea kwa kasi isiyobadilika, tunahisi kana kwamba haisafiri katika anga.

Kila kitu duniani, ikiwa ni pamoja na wanadamu, husafiri kwa kasi hii ya mara kwa mara, tunazunguka na sayari, ila hatuhisi safari hiyo.

Lakini kuna mambo mengine muhimu.

Image: BBC

Maelezo ya picha,Mvuto wa sumaku ya dunia pia huturuhusu kutohisi mienendo ya mara kwa mara ya Dunia

Nguvu nyingine ambayo pia ina jukumu

Unaweza pia kusoma:Fahamu kituo cha kwanza cha anga za mbali chenye usiri mkubwa4 Disemba 2021

Nguvu ya sukamu ya dunia pia inaeleza kwa nini hatuhisi Dunia ikizunguka.

"Fikiria ukiingia kwenye gari la Formula 1 na kusafiri katika mstari ulionyooka kwa kasi isiyobadilika," anasema Solmar Varela, mwanafizikia wa kinadharia na mwanasayansi maarufu katika Chuo Kikuu cha Kati cha Venezuela.

“Wakati huo hutasikia gari likisogea, lakini ukifika kwenye kona utahisi nguvu ikikusukuma kuelekea upande wa pili wa kona, kana kwamba inajaribu kukutoa nje ya gari kwa nguvu,” anaeleza Bw. Varela.

"Sababu ya kutotupwa kutoka kwa gari ni kwa sababu umefunga mkanda," anaongeza.

Vivyo hivyo kwa sayari yetu. Inapozunguka, hutoa nguvu ya sumaku ambayo, kwa nadharia, inapaswa kutuumiza angani.

Lakini nguvu ya sumaku ya Dunia ina nguvu zaidi kuliko nguvu hii ya katikati, na kwa hivyo tunabaki kushikamana na sayari.

"Mvuto wa sumaku hufanya kazi kama ya mkanda wa usalama wa gari," anaeleza Bw. Varela.

Kusonga kunategemea mahali ulipo

Image: BBC

Maelezo ya picha,Kutokuwa na uwezo wetu wa kutambua harakati za Dunia ni moja ya sababu kwa nini, kwa karne nyingi, iliaminika kuwa nyota zinazunguka sayari yetu

Hisia kwamba Dunia haizunguki ilikuwa mojawapo ya sababu zilizofanya, kwa karne nyingi, sayari yetu iaminike kuwa kitovu cha ulimwengu.

“Kwa muda mrefu, iliaminika kwamba Dunia ndiyo kitovu cha ulimwengu, kwa sababu watu walipotazama angani, waliona kwamba nyota ndizo zinazosonga,” anaeleza mtaalamu wa nyota wa Venezuela Miriam Rengel, mtafiti katika Max Planck, ambayo ni Taasisi ya utafiti juu ya mfumo wa jua nchini Ujerumani.

“Lakini mambo yalibadilika Nicolaus Copernicus na Johannes Kepler walipotengeneza kielelezo cha heliocentric na Galileo kugundua miezi minne ya Jupiter na kuona kwamba hizo ndizo sayari zinazozunguka Jua,” aongeza Miriam Rengel.

Wanaoamini wazo kuwa dunia ipo katikati ya ulimwengu (geocentrism) walisema kwamba ikiwa sayari ingesonga, tutaihisi, na kwamba ikiwa tungeangusha kitu kutoka mahali pa juu, kitatua sio chini, lakini nyuma yake.

Lakini Galileo alipata njia ya kukanusha hoja hizo.

Alifanya majaribio kwenye boti iliyokuwa ikisafiri kwa mwendo wa kasi katika bahari tulivu na kumimina tone la maji kwenye chombo.

Kisha akagundua kwamba, ingawa mashua ilikuwa inasonga mbele, bado matone yalikuwa yakianguka kwenye kontena.

“Alionyesha kwamba kila kitu kinategemea mahali ulipo,” anaeleza Bw. Rengel.

Kwa hivyo Galileo alikuwa wa kwanza kuunda kanuni ya uhusiano.

Image: BBC

Maelezo ya picha,Uchunguzi wa Galileo ulifunua kwamba Dunia ilizunguka na kuzunguka Jua.

Mazoea na kuandaliwa

Sababu nyingine kuhusu ni kwa nini hatuwezi kutambua harakati za Dunia ni kwamba tumeizoea tu.

"Tumezoea harakati za mzunguko wa dunia tangu tulipozaliwa," anaeleza Marta Ábalos, profesa wa fizikia ya dunia katika Chuo Kikuu cha Complutense cha Madrid.

Kwa upande wake, Rey anasisitiza kuwa mfumo wa kusikia wa viumbe hai umebadilika ili kuzuia harakati za sayari kutufanya tupate kizunguzungu, kwa mfano.

Ukweli kwamba anga ya hewa hutembea kwa takriban kasi sawa na Dunia pia ina changia

Wakati safu ya hewa inayozunguka Dunia inazunguka kwa karibu kasi sawa, hatuhisi 'upepo' wowote kutokana na mzunguko wa Dunia," anasema Ábalos.

Zaidi ya hayo, kulingana na Rey, harakati za sayari hazitoi upepo kwa sababu "nafasi ni tupu."