Watengezaji bidhaa Kenya watishia kusitisha shughuli kupinga msuada wa fedha 2024

KAM imesema wakenya watarajie hali ngumu ya maisha kwa kuwa bei za bidhaa muhimu hasa mafuta, simiti, chuma na nepi zkitarajiwa kupanda.

Muhtasari

• Washikadau wa muungano wa watengezaji bidhaa wametishia kusitisha shughuli zao humu nchini

 


Serikali yaitengea KRA pesa za kuajiri majasusi kuwafuatilia wanaokwepa kulipa ushuru.
Serikali yaitengea KRA pesa za kuajiri majasusi kuwafuatilia wanaokwepa kulipa ushuru.
Image: FACEBOOK

Munngano wa watengenezaji bidhaa nchini Kenya (KAM) umetishia kusitisha shughuli zao humu nchini kupinga msuada wa Kifedha 2024 .

Aidha,wametishia kufunga shughuli zao nchini Kenya na kutafuta njia mbadala za kibiashara katika nchi jirani ya Tanzania iwapo mswada huu utapitishwa.

Kulingana na muungano huo, wakenya watarajie hali ngumu ya maisha kwa kuwa bei za bidhaa muhimu hasa mafuta, simiti, chuma na nepi  zkitarajiwa kupanda.

’’Bunge liwe na utu hasa katika kutoza ushuru wa vyakula. Vilevile liwe makini sana hasa katika taifa ambalo takriban asilimia thelathini ya watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano wanakosa lishe bora,’’ alisema mwanachama wa muungano huo.

‘’Wafanyikazi wengi watapoteza kazi. Ukitazama kwa kawaida,huwa tunao wafanyikazi mia moja na thelathini na tukiwapunguza kwa asilimia kumi ama kumi na tano hiyo itakuwa takriban wafanyikazi ishirini na hiyo itakua na athari kubwa sana,’’ alisema mumiliki wa mkahawa Nairobi, Obado Obado.

Wakenya wanaelezwa kutarajia hali ngumu ya maisha iwapo mswada wa kifedha wa mwaka 2024/2025 utapitishwa na bunge.

Vilevile, serikali ilipendekeza kutozwa kwa ushuru kwa magurudumu ya mpira ambapo gurudumu moja la toroli litapanda bei kutoka shilingi elfu moja hadi shilingi elfu moja na mia saba kuashiria hali ngumu inayomngoja 'Hustler'. 

Tetesi za mswada huu wa kifedha umezidi kuibua hisia mbalimbali miongoni mwa wakenya huku athari zake zikionekana bayana.