Wanawake wa zamani walikuwa na mtazamo gani kuhusu ngono?

Ikiwa tungechukua maelezo kama hayo, tungefikia hitimisho kwamba wanawake zamani walikuwa wapenda ngono.

Muhtasari

•Idadi kubwa ya maandishi ya mwanzo yaliandikwa na wanaume ambao walikuwa na tabia ya kuzidisha tabia za kijinsia za wanawake katika namna mmoja au nyingine.

Image: BBC

Kitabu kipya kinaelezea historia ya ulimwengu wa kale kupitia wanawake. Mwandishi Daisy Dunn anachunguza walichosema kuhusu jinsia yao wenyewe - mbele ya dhana potofu za wanaume.

Kulingana na Semonides wa Amorgos, mshairi wa kiume alieishi Ugiriki katika Karne ya 7 KK, kuna aina 10 kuu za wanawake. Wanawake ambao ni kama nguruwe, kwa sababu wanapendelea kula kuliko kufanya usafi.

Wanawake wanaofanana na mbweha, wao ni waangalizi tu; wanawake kama punda, hao ni wazinzi, wanawake mbwa, hawa wana alama kwa uasi wao.

Vilevile, kuna wanawake wa dhoruba ya baharini, ni wale wenye tamaa, wanawake wezi, wanawake wavivu, wanawake wasiovutia, na - aina moja nzuri – wanawake nyuki, wanaofanya kazi kwa bidii.

Kati ya wanawake wote walioelezewa katika orodha hii, ambayo inaakisi upotovu wa wakati huo, wale wanaoitwa "wanawake-punda" yaani wapenda uzinzi, labda ndio wa kushangaza zaidi.

Idadi kubwa ya maandishi ya mwanzo yaliandikwa na wanaume ambao walikuwa na tabia ya kuzidisha tabia za kijinsia za wanawake katika namna mmoja au nyingine.

Wengine kwa makusudi waliwaonyesha wanawake kama wapenda ngono kama njia ya kuwachafua wahusika wao. Ikiwa tungechukua maelezo kama hayo, tungefikia hitimisho kwamba wanawake zamani walikuwa wapenda ngono.

Jinsi ukahaba ulivyoonekana

Ukitembelea danguro la kale, kama lile la Pompeii, ili kuona namna ngono ilivyokuwa. Kuta za vyumba, ambamo wafanyabiashara ya ngono walifanya biashara yao, zimeandikwa na wateja wa kiume, ambao walitoa maoni yao kuhusu maonyesho ya wanawake hao.

Dhidi ya Neaera, hotuba ya mashtaka iliyotolewa na mwanasiasa wa Athene, Apollodorus katika Karne ya 4 KK, inatoa ufahamu wa kushangaza kuhusu hatari iliyowakumba wanawake hawa.

Katika Karne ya 3 KK, mshairi wa kike anayeitwa Nossis, aliyeishi Italia aliandika kwa kusifu kazi ya sanaa - ambayo kiukweli ilikuwa imeandaliwa na mfanyabiashara wa ngono.

Sanamu tukufu ka Aphrodite, mungu wa kike wa ngono na upendo, aliyeimbwa na Nossis, ilikuwa imesimamishwa katika hekalu kwa kutumia pesa zilizokusanywa na Polyarchis.

Mawazo ya wanaume

Waandishi wa kiume, licha ya chuki zao, wanaweza kutoa maelezo ya kuvutia kuhusu wanawake na ngono. Mwaka 411 KK, mchekeshaji Aristophanes aliigiza mchezo unaoitwa Lysistrata.

Ambapo wanawake wa Athene wanafanya mgomo wa ngono kwa nia ya kuwashawishi waume zao kukubaliana na masharti ya amani wakati wa Vita vya Peloponnesian.

Huu ulikuwa mzozo wa kweli, ulioanzishwa kati ya Athene na Sparta na washirika wao kwa miongo mitatu. Wanawake wengi kwenye tamthilia walifurahia kuacha raha zao.

Mhusika mkuu Lysistrata, ambaye ndiye anayepanga mgomo huo, anaelezea jinsi wanawake walivyo wakati wa vita.

Sio tu kwamba wamepigwa marufuku katika Bunge, ambalo vita hujadiliwa, lakini mara kwa mara wanafiwa. Ingawa mgogoro huo wa muda mrefu ni mbaya kwa wanawake walioolewa, ni mbaya zaidi kwa wanawake ambao hawajaolewa, ambao wananyimwa nafasi ya kuolewa.

Ingawa wanaume hao, Lysistrata anasema, huenda wakarudi nyumbani kutoka vitani wakiwa na mvi na bado wanaweza kuoa, hali haiku hivyo kwa mabikira, ambao wengi wao watahesabiwa ni wazee sana kuolewa na kuzaa.

Hadithi hii inawasilisha tofauti ya athari za vita kwa wanaume na wanawake. Inaakisi kwa usahihi, kile ambacho wanawake wa siku hizo walikuwa wakikisema.

Sophocles, mwandishi wa tamthilia maarufu Oedipus Rex, mhusika wa kike katika tamthilia akiitwa Tereus anaelezea jinsi inavyokuwa kutoka kuwa bikira hadi kuwa mke.

Ilikuwa ni kawaida kabisa miongoni mwa watu wa tabaka la juu kupanga ndoa. Siku ya kwanza kwa mwanamke kujamiiana inaweza kuwa ya kuogopesha.

Kuhusu ngono ya kale

Mchoro wa Victoria Aubrey Beardsley taswira ya Lysistrata kwa toleo lililochapishwa la vichekesho vya Aristophanes kuhusu wanawake wa Athene wakigoma kufanya ngono
Mchoro wa Victoria Aubrey Beardsley taswira ya Lysistrata kwa toleo lililochapishwa la vichekesho vya Aristophanes kuhusu wanawake wa Athene wakigoma kufanya ngono
Image: BBC

Katika barua inayohusishwa na Theano, mwanafalsafa wa kike Mgiriki, katika mazungumzo na Pythagoras (wengine wanasema alikuwa mume wake), anampa rafiki yake Eurydice ushauri muhimu.

Anaandika, “mwanamke anapaswa aondoe aibu yake pamoja na nguo zake anapoingia kwenye kitanda cha mumewe. Anaweza kuzriudisha zote mbili mara tu anaposimama tena.”

Barua ya Theano inaangazia kwa ukaribu yale ambayo wanawake wengi wameambiana, na ushauri wake unaonekana kufuatwa na wanawake katika ulimwengu wa sasa pia.

Mshairi fulani wa Kigiriki, Elephantis, alikuwa na hamu sana ya kuwapa wanawake ushauri kuhusu mambo ya ngono na aliandika vitabu vyake vifupi kuhusu mada hiyo.

La kusikitisha hakuna kazi yake leo, lakini zinatajwa na mshairi wa Kirumi Martial na mwandishi wa wasifu kutoka Roma, na mtunzi wa kumbukumbu Suetonius, ambaye alidai kwamba Mfalme Tiberius (aliyejulikana sana kwa kupenda ngono) alikuwa na nakala.

Wanawake wengine wamenukuliwa katika maandishi ya wanaume, wakieleza suala la upendo na sio ngono waziwazi, ambapo ni tofauti na baadhi ya wanaume wa rika zao, ikiwa ni pamoja na Martial na Catullus.

Mpenzi asiyejulikana wa Catullus, anamwambia, "kile mwanamke anachosema kwa mpenzi wake wakati huu, kinapaswa kuandikwa kwenye upepo na maji yanayobubujika".

Sulpicia, mmoja wa washairi wachache wa Kirumi ambao beti zao zipo, anaelezea masaibu yake ya kuwa mashambani mbali na mpenzi wake Cerinthus katika siku yake ya kuzaliwa.

Wanawake hawa hawakuhitaji kuelezea ngono ili kufichua kile walichofikiria juu ya ngono. Wanaume wanaweza kutawala hadhira lakini wanawake, kama Aphrodite alijua vizuri, wanaweza kutawala wakati mapazia yanapofungwa.