Najutia kuavya mimba wiki moja kabla ya harusi yangu- Mwanamke asimulia yaliyojiri

Haya ni matamshi ya mwanamke mmoja ambaye alisimulia jinsi anajutia kuavya mimba kabla ya harusi yake.

Muhtasari
  • Kama kawaida kama vijana lazima tujihusishe kwenye tendo la ndoa kabla ya kuoana kamili, na nina uhakika sio mimi na mume wangu tumefanya hayo kabla ya ndoa.
Mwanamke mwenye huzuni
Mwanamke mwenye huzuni
Image: HISANI

Wengi wamekuwa wakishanga kwanini sijaweza kupata mtoto licha yangu kuwa kwenye ndoa kwa miaka 12.

Ni siri ambayo nimekuwa nimeficha na kuweka nikiwa na mume wangu wakati huo wote.

Kama kawaida kama vijana lazima tujihusishe kwenye tendo la ndoa kabla ya kuoana kamili, na nina uhakika sio mimi na mume wangu tumefanya hayo kabla ya ndoa.

Haya ni matamshi ya mwanamke mmoja ambaye alisimulia jinsi anajutia kuavya mimba kabla ya harusi yake.

Nikiwa kwenye pilkapilka zangu nilikutana na  Dorcas ambaye alinisimuliajinsi amekuwa akitafuta mtoto ili ndoa yake iwe na amani kwa zaidi ya miaka 10.

Kulingana na Dorcas watu wengi walisikilia wivu uhusiano wake na mumewe huku wakiutaja, na kuwaita 'perfect couples' lakini hawakufahamu walichokuwa wanapitia katika ndoa yao.

Baada ya wenzi wawili kufunga ndoa ni matarajio ya wengi kwamba baada ya fungate, lazima wawe wamefanya jambo na wanatarajia mtoto, lakini haya hayakuwa kwa Dorcas kwani hakufahamu baada ya kuavya mimba kabla ya harusi yake kuliharibu tumbo la uzazi wake.

Hii hapa hadithi yake;

"Wakwe wangu walinikubali kwa mikono yote na kunipenda, lakini hawakufurahishwa na kisa changu cha kutowapatia wajukuu au angalau mjukuu mmoja.Nilidhani kuwa nitakuwa na furaha kama wanandoa wengine kwani nilijua nina uwezo wa kubeba mimba

Lakini kile najutia zaidi ni kuwa nisingeavya ujauzito wangu wiki moja kabla ya harusi yangu, kwa sababu baada ya miezi chache kwenye ndoa nilienda kumuona dakatari na alinipa habari za kuhuzunisha kuwa mfuko wangu wa uzazi uliharibika

Baada ya kupata matibabu nilibeba ujauzito wa kwanza lakini uliharibika kwa maana mfuko wangu haungeweza kustahimili ujauzito huo

Ndio mume wangu anajua na kufahamu vyema kwamba niliavya mimba kwani yeye na msimamizi wangu wa harusi ndio walinishauri niweze kuavya ili kuepuka maswali mengi ya watu baada ya harusi, lakini ningejua singewesikiza

Kile naweza kuwashauri vijana wa sasa ni kuwa ukipata mimba msikuwa na haraka ya kuamua jambo fulani, na jambo ambalo litawaleta madhara katika maisha ya baadaye na wasiogope kuongewa na watu kama nilivyofanya lakini najutia peke yangu

Kwa hivyo wakue makini kwa kila jambo wanalolifanya."