Inasikitisha! Video ya msichana mdogo akivuka daraja hatari chini ya mto uliofurika yazua hisia

Eric Omondi ametangaza kuwa anamtafuta msichana huyo na familia yake ili aweze kuwasaidia kuhamia mahali salama.

Muhtasari

•Msichana huyo mdogo anaonekana akijaribu kusalia imara kwa kujishikilia kwenye miti iliyowekwa kando ya daraja hilo  huku akivuka kwa umakini.

•Eric Omondi amewakashifu wanasiasa kwa kulegeza wajibu wao wa kujenga na kuboresha miundombinu kama vile daraja.

akivuka daraja hatari
Mtoto akivuka daraja hatari
Image: HISANI

Video ya msichana mdogo ambaye bado hajatambulika akivuka daraja jembamba sana juu ya mto uliojaa kupita kiasi wakati akielekea shuleni imesambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Katika video hiyo ambayo imezua hisia mseto kutoka kwa Wakenya kwenye mitandao ya kijamii, msichana huyo mdogo anaonekana akijaribu kuwa imara kwa kujishikilia kwenye miti iliyowekwa kando ya daraja hilo jembamba huku akivuka kwa umakini.

Msichana huyo alivalia sare ya shule ya buluu iliyokolea na begi mgongoni. Alionekana kuruka kutoka kwenye daraja na kupata utulivu anapomaliza kuvuka mto huo unaoonekana kuwa hatari chini yake.

Mmoja wa watu ambao wametoa sauti zao kuhusu video hiyo ni mchekeshaji Eric Omondi ambaye amewakashifu wanasiasa kwa kulegeza wajibu wao wa kujenga na kuboresha miundombinu kama vile daraja.

Mchekeshaji huyo alibainisha kuwa kwa kuvuka daraja hilo hatari, msichana huyo anakabiliwa na hatari ya kifo kwani mto ulio chini yake unaweza kumuua iwapo angeanguka.

“Hawa viongozi wanalalaje hata usiku??? Kwa hiyo msichana huyu mdogo anakabili kifo kila asubuhi. Akipiga hatua moja ndogo ya kukosea ndivyo hivyo😡, TUNAMPOTEZA!!! Huyu mtoto anaweza kupoteza maisha kwa sababu tu ya KIONGOZI MWENYE TAMAA, MTUKUFU na MUUAJI!!!” Eric Omondi alisema.

Aliendelea kutangaza kwamba anamtafuta msichana huyo mdogo kwenye video hiyo na familia yake ili aweze kuwasaidia kuhamia mahali salama.

“Namtafuta huyu Msichana, inabidi tumuokoe. Tutamleta yeye na familia yake Nairobi. HATA KUVUKA TENA hili DARAJA LA MAUTI. Tafadhali TUMPATE. Ikiwa unatambua mahali hapa tafadhali toa maoni yako au tuma DM MAHALI.,” Eric alisema.

Wanamtandao wameendelea kuguswa na video hiyo huku watu tofauti wakiwemo wanasiasa, wazazi, majirani, mtu aliyerekodi video hiyo miongoni mwa wengine wakikosolewa kuhusu hali hiyo.

Tazama maoni ya baadhi ya Wakenya;-

@You_and_i_fashionke: A bridge construction would be far better cos I guess there are 100’s of lives being risked here presidente. If for a bridge am in.

@janekabutha49: You will save her..but who will save the rest?

@milkahdee: Start with her mom then leaders how dare awache mtoto apite hapo mama yake afaakushikwa aki

@elishajames: How about the guy who’s recording,he could ensure that the kid passes safely

@musyoki8906: Hapa ni kisii county, bassi bogetario ward, mca ni machuki.