BBI ni ndoto iliyoahirishwa-Rais Uhuru asema wakati wa sherehe za Jamhuri

Muhtasari
  • Rais Uhuru Kenyatta amekariri kwamba marekebisho ya katiba ya Building Bridges Initiative ni ndoto ambayo itaafikiwa
Rais Uhuru Kenyatta wakati wa sherehe za Jamhuri
Image: Mercy Mumo

Rais Uhuru Kenyatta amekariri kwamba marekebisho ya katiba ya Building Bridges Initiative ni ndoto ambayo itaafikiwa.

Akizungumza Jumapili, wakati wa sherehe za Jamhuri, rais alisema kuwa Wakenya wanafaa kuungana na kurekebisha nyufa kwenye kuta za taifa letu.

“Hili naamini ndilo lililolazimu marekebisho ya kwanza ya katiba yetu,” Uhuru alisema.

"BBI ni ndoto iliyoahirishwa siku moja, siku moja itatokea."

Huku akizungumzia bustani ya Uhuru alisema kwamba itakuwa kitabu cha historia.