(+PICHA)Vijana wazua ghasia huku wakijaribu kukatiza mapokezi ya Mudavadi Bomas

Muhtasari
  • Vijana wazua ghasia huku wakijaribu kukatiza mapokezi ya Mudavadi Bomas
Image: Wilfred Nyangaresi

Kulikuwa na fujo baada ya baadhi ya vijana kujaribu kuzuia mapokezi ya kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi katika ukumbi wa Bomas of Kenya.

Wanaume walionekana wakipigana huku vumbi likikodi hewa.

Polisi pia walionekana wakiwa wamebeba bunduki zao huku wakikimbia kuelekea kwenye mtafaruku huo.

Kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi anatazamiwa kuzindua azma yake ya urais katika ukumbi wa Bomas of Kenya leo.

Image: Wilfred Nyangaresi

Mudavadi amewaambia wafuasi wake wajiandae kutangaza tangazo kuu, litakalompa mamlaka ya kuongoza na kushiriki katika mpangilio wowote wa muungano utakaofaidi Wakenya na chama.

Chama hicho pia kinatarajiwa kufichua ‘marafiki zake wa kisiasa’ wakati wa mkutano huo.

Hizi hapa baadhi ya picha za machafuko hayo;

Image: Wilfred Nyangaresi
Image: Wilfred Nyangaresi
Image: Wilfred Nyangaresi