'Alichinjwa kama Ng'ombe,'Mkewe Isaac Juma asimulia jinsi mumewe alivyouawa

Muhtasari
  • Mkewe shabiki mkongwe wa Harambee Stars Isaac Juma amesimulia jinsi mumewe aliuawa kwa kukatwakatwa
Isaac Juma
Image: Hisani

Mkewe shabiki mkongwe wa Harambee Stars Isaac Juma amesimulia jinsi mumewe aliuawa kwa kukatwakatwa.

"Tulikuwa tukila chakula cha jioni nyumbani kwetu na kabla ya kulala, tulisikia kondoo wakilia kwenye shamba letu," alisema.

Akizungumza na KTN siku ya Alhamisi, Farida alisema Juma aliondoka nyumbani kwenda kuangalia tatizo lilikuwa wapi.

"Lakini walipofungua mlango, wanaume hao walikuwa wakimngoja juu ya mti," alisema kwa njia ya kitamathali huku akielekeza kwenye mti uliokuwa nyuma yake.

"Alipiga mayowe kuomba msaada alipowaona wanaume hao. Niliposikia zogo, niliamka haraka na kumkuta mume wangu mikononi mwa washambuliaji," alisema.

Alisema washambuliaji walikuwa tayari wametoroka kutoka nyumbani.

“Alikuwa akikata shingo mithili ya mtu anayechinja ng’ombe, aliponiona naye alikimbia,” alisema.

"Aliniambia alikuwa na masuala ya ardhi katika eneo hilo, na ikitokea kifo chake, niwaambie mamlaka kwamba ni kwa sababu ya mgogoro wa ardhi."

Polisi walisema wamemkamata mshukiwa kuhusu shambulio hilo.

Maafisa wanaoshughulikia suala hilo walisema matokeo ya awali yameonyesha shambulio hilo lilitokana na mzozo wa ardhi katika eneo hilo.

Kutoka kwetu wanajambo Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.