Watuhumiwa wa mauaji wasafirishwa Uingereza

Muhtasari

• Makachero kutoka kitengo cha DCI wametangaza kuwasafirisha watuhumiwa wawili wa mauaji kwenda Uingereza ili kujibu mashtaka.

• Washukiwa hao wawili walikuwa wametoroka baada ya kufanya mauaji na walikamatwa nchini Januari 26 baada ya msako mkali dhiti yao.

Mohamud Siyad Abdihakim, Monteiro Tariq Kennedy Mangal na kisu
Image: DCI (Facebook)

Makachero kutoka kitengo cha DCI wametangaza kuwasafirisha watuhumiwa wawili wa mauaji kwenda Uingereza ili kujibu mashtaka.

Washukiwa hao wawili walikuwa wametoroka baada ya kufanya mauaji na walikamatwa nchini Januari 26 baada ya msako mkali dhiti yao.

Watoro hao Mohamed Siyad Abdihakim ,24 na Monteiro Tariq Kennedy Mangal, 21, ambao wote ni raia wa Uingereza walikamatwa katika mtaa wa Kilimani jijini Nairobi kufuatia taarifa za kijasusi zilizoelekeza maafisa wa upelelezi wa uhalifu wa kimataifa.

Awali, hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa wawili hao ilikuwa imetolewa kufuatia mauaji ya Alex Smith, 16, kutoka kaskazini mwa London mwaka wa 2019. Mauaji ambayo wawili hao wanashukiwa kuhusika kabla ya kuabiri ndege na kutoroka kusikojulikana.

Taariifa za kijasusi kutoka kwa polisi wa mjini ambao wamekuwa wakiwasaka watuhumiwa hao zinasema kuwa wanaamini mmoja wa watoro hao alihusika katika kumfuma kisu kijana Smith huku mwingine akihusika kama dereva aliyekuwa akiliendesha gari la wizi ambalo walitumia siku hiyo ya tukio.

Tangu kutorokea kwao nchini, wawili hao wamekuwa mafichoni katika mtaa wa Kilimani jijini Nairobi huku wakitumahi kwamba watakwepa mashtaka dhidi ya mauaji nchini mwao huko Uingereza.

Wakati wa kukamatwa kwao, mshukiwa Kenedy alipatikana na umilisi wa kitambulisho cha nchi Jirani ya Somali kilichosajiliwa kwa jina la Abdulahi Abshir Mohamed Pamoja na kisu.

“Wawili hao tayari washasafirishwa kuelekea Uingereza ili kujibu mashtaka na familia ya kijana Smith inatarajia kupata haki,” taarif ya DCI ilisema.