Mbunge Barasa nchini Uganda baada ya madai ya mauaji-polisi

Nasokho alitangazwa kufariki katika Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Kimilili.

Muhtasari
  • Bosi huyo wa polisi alisema Barasa anajua anasakwa kutokana na tukio hilo lakini alichagua kuzima simu yake na kutoroka
Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa
Image: MAKTABA

Polisi wanaamini kuwa Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa alitorokea Uganda baada ya madai ya kuua msaidizi wa mpinzani wake Siku ya Uchaguzi.

Polisi wanaoshughulikia tukio hilo walisema mbunge huyo kufikia Jumatano alikuwa hajasalimisha kama alivyoagizwa.

Barasa, ambaye anatetea kiti chake kwa tikiti ya UDA, ni mmiliki wa bunduki aliyeidhinishwa.

Kisa hicho kilihusisha Barasa na mpinzani wake wa kisiasa Brian Khaemba wa DAP katika kituo cha kupigia kura cha Chebukwabi ambapo walipaswa kushuhudia kuhesabiwa kwa kura.

Afisa wa Upelelezi wa Jinai katika Kaunti ya Bungoma Joseph Ondoro alisema mkasa ulitokea wakati ugomvi ulipozuka kati ya wawili hao na kumfanya Khaemba kuondoka na kuelekea kwenye gari lake.

“Barasa alimfuata akiwa na watu wanne na kuwaamuru wasimruhusu (Khaemba) kuondoka mahali hapo. Hata hivyo, dereva wa Khaemba Joshua Nasokho alikaidi agizo hilo na kuwasha gari hilo,” Ondoro alisema.

Hapo ndipo Barasa anaripotiwa kuchomoa bastola.

Nasokho alitangazwa kufariki katika Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Kimilili.

Ondoro alisema wanamtafuta Barasa kuhusu tukio hilo.

“Amekimbia lakini tunamtafuta. Ajisalimishe,” alisema.

Ondoro alisema walianzisha msako wa kuwasaka watu lakini bado wanasaka maeneo yote ambayo Barasa huenda amejificha.

“Tunashuku alichukua pikipiki kuelekea Uganda lakini tutampata. Bado hajakamatwa,” alisema Jumatano.

Bosi huyo wa polisi alisema Barasa anajua anasakwa kutokana na tukio hilo lakini alichagua kuzima simu yake na kutoroka.

Eneo ambalo kisa hicho kilitokea ni karibu na mpaka wa Kenya na Uganda.

Timu ya waunga mkono imetumwa eneo hilo kumtafuta mbunge huyo.

Katika eneo bunge la Malava, polisi walisema walimzuilia mgombeaji ubunge Seth Panyako na wafuasi 12 katika kituo cha kupigia kura cha Maira, kutokana na machafuko yaliyotokea huko.

Walishtakiwa kwa kuwashikilia maafisa wa uchaguzi kabla ya polisi kuwaokoa na kuwapeleka katika kituo cha polisi cha Kabras.

Polisi walipanga kuwafungulia mashtaka mbalimbali.