Mutahi Ngunyi amjibu mwanawe Museveni kuhusu vitisho kwa Kenya

"Mapinduzi ni kama Covid, yanaenea. Nchini Kenya Ruto yuko salama. Lakini je Uganda iko salama?"

Muhtasari
  • Mutahi alifananisha kuondolewa madarakani na janga hili, akishangaa ikiwa Uganda ilikuwa salama dhidi ya ugonjwa huo

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Mutahi Ngunyi ametilia maanani matamshi yaliyotolewa na mwanawe Rais wa Uganda Yoweri Museveni Muhoozi Kainerugaba jinsi ya kuteka Nairobi.

Alisema kauli hiyo ilichochewa na mapinduzi yaliyoathiri mataifa mbalimbali barani humo.

"Jinsi ya kusoma Siasa 101. Wakati Uganda inachokoza Nairobi bila sababu nzuri za kidunia, kuna mapinduzi nchini Burkina Faso, jaribio la kukabiliana na mapinduzi nchini Mali, Guinea Bissau, Chad na Sudan," aliandika Jumatatu.

Mutahi alifananisha kuondolewa madarakani na janga hili, akishangaa ikiwa Uganda ilikuwa salama dhidi ya ugonjwa huo.

"Mapinduzi ni kama Covid, yanaenea. Nchini Kenya Ruto yuko salama. Lakini je Uganda iko salama?"

Katika mfululizo wa jumbe siku ya Jumatatu, Kainerugaba alidai yeye na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda (UPDF) wanaweza kuchukua udhibiti wa Nairobi chini ya wiki mbili.

"Haingetuchukua sisi, jeshi langu na mimi, wiki 2 kukamata Nairobi," alitweet.

Katika tweet nyingine, alikejeli kipengele cha kikatiba cha Kenya cha ukomo wa mihula ya urais akisisitiza kwamba hiyo haifanyi kazi kwa Uganda.