Kalonzo amtaka Ruto kutafakari upya msimamo wake kuhusu GMO

Kuondolewa kwa marufuku iliyowekwa mwaka wa 2012 kutaruhusu wakulima kupanda mimea iliyotengenezwa kijenetiki.

Muhtasari

• Oktoba 3, rais Ruto aliondoa marufuku ya mazao ya GMO ambayo iliwekwa mwaka wa 2012.

Alisema alifuata mapendekezo ya Kikosi Kazi kilichoundwa Kupitia Masuala Yanayohusu Vyakula vya kiteknolojia  na Usalama wa Chakula.

Kiongozi wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka akihutubia wanahabari jijini Nairobi Oktoba 11, 2022.
The star Kiongozi wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka akihutubia wanahabari jijini Nairobi Oktoba 11, 2022.
Image: The star

Shinikizo za wanaomtaka Rais William Ruto kufikiria upya msimamo wake wa kuondoa marufuku ya vyakula vya GMO nchini zinazidi kuimarisha.

Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka ndiye kiongozi wa hivi punde zaidi kumtaka Rais kutafakari upya msimamo wake kuhusu suala hilo akisema vyakula vya GMO vitapunguza uhaba wa chakula nchini lakini hatimaye wananchi wataathirika kiafya.

"Wakati Rais alipokuwa Waziri wa Kilimo, alipinga vikali GMO kama mimi... Ninatoa wito kwa William kufikiria upya (kuondoa marufuku) kwa ajili ya nchi hii," Kalonzo alisema.

Alisema alifuata mapendekezo ya Kikosi Kazi kilichoundwa Kupitia Masuala Yanayohusu Vyakula vya kiteknolojia  na Usalama wa Chakula.

Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumanne, Kalonzo alisema kuwa chakula cha GMO kitasababisha matatizo kuuza mazao yetu katika nchi jirani huku ikizingatiwa kwamba nchi nyingi katika hii hazikubali vyakula vya GMO. 

"Hata kama wakulima wetu watatumia mbegu ya mahindi aina ya BT, hii haitapunguza gharama ya mahindi kwa kuwa bei inabadilishwa kiholela," aliongeza.

Kalonzo aliongeza kuwa usalama wa chakula haufai kutegemea matumizi ya mahindi pekee.

Kiongozi wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka akihutubia wanahabari jijini Nairobi Oktoba 11, 2022.
Kiongozi wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka akihutubia wanahabari jijini Nairobi Oktoba 11, 2022.
Image: The star

Huku akilaani uamuzi wa kuondoa marufuku hiyo, Kalonzo alitoa wito kwa Kanisa kuzungumzia swala hili .

 "Tunashangazwa na ukimya wa Kanisa ambao wakati fulani ulikuwa dhidi ya GMOs. Je, inawezekana wametulizwa na utawala mpya... tunawasihi viongozi wetu wa dini wasiuze roho zao bali wazungumze ukweli madarakani," alisema.

Kuondolewa kwa marufuku iliyowekwa mwaka wa 2012 sasa kutaruhusu wakulima kupanda mimea iliyotengenezwa kijenetiki na vyakula vya mifugo.

Hii inatarajiwa kuongeza uzalishaji wa chakula na mifugo nchini.

Hata hivyo, mazao haya ya technolojia kwa ujumla yameibua wasiwasi kuhusu madhara yanayoweza kuathiri mashamba ya wakulima wadogo, mazao yaliyopo, mazingira na afya ya muda mrefu ya watu.

Image: EZEKIEL AMING'A