Msiwaburute watumishi wa umma kwenye siasa, DP Rigathi aonya

"Serikali ya William Ruto haitatumia machief na macounty commisisoner kwa mambo ya siasa. Hio hapana kazi yao."

Muhtasari
  • Alisema maafisa wa polisi ni sehemu muhimu ya nchi lakini wanatumiwa kwa sababu zisizo sahihi kisiasa
Naibu Rais William Ruto
Image: TWITTER// RIGATHI GACHAGUA

Naibu Rais Ragathi Gachagua amewaonya wanasiasa dhidi ya kutumia maafisa wa polisi na watumishi wengine wa umma kwa madhumuni ya kisiasa.

Akizungumza Jumatatu alipokuwa akiongoza Maadhimisho ya Kila Mwaka ya Siku ya Chakula Duniani katika Kaunti ya Kajiado, DP alisema machifu na makamishna wanapaswa tu kufanya kile wanacholipwa.

"Serikali ya William Ruto haitatumia machief na macounty commisisoner kwa mambo ya siasa. Hio hapana kazi yao."

Alisema maafisa wa polisi ni sehemu muhimu ya nchi lakini wanatumiwa kwa sababu zisizo sahihi kisiasa.

Gachagua alisema kuwa utawala wa Kenya Kwanza ulipata mamlaka ya kisiasa bila usaidizi wa polisi na machifu.

"Rais na mimi tumeweka wazi. Tutasimamia siasa zetu wenyewe. Hatuhitaji polisi, hatuhitaji DCI, hatuhitaji KRA, hatuhitaji chombo chochote cha serikali kusimamia shughuli zetu. siasa. Tutasimamia siasa sisi wenyewe," Gachagua alisema.

Wakati wa kampeni, Gachagua na kundi zima la Kenya Kwanza walidai kuwa utawala wa Jubilee ulikuwa ukitumia wasimamizi kumfanyia kampeni mgombeaji wa Azimio Raila Odinga.

Mnamo Jumapili, Rais William Ruto pia alidai kuwa kitengo cha DCI kilichokuwa kikitumiwa na utawala uliopita kuwaua Wakenya kimevunjwa.