Nina thamani ya Sh101 milioni-Waziri mteule wa Afya Susan Wafula

Wafula alizungumza alipofika mbele ya Kamati ya Bunge ya Kitaifa kuhusu Uteuzi katika Jumba la Kaunti, Nairobi.

Muhtasari
  • Aliwaambia wabunge wanaowahoji Mawaziri wateuliwa Jumatano mali zake nyingi ziko katika mfumo wa ardhi iliyoenea katika kaunti nne
SUSAN WAFULA
Image: EZEKIEL AMING'A

Waziri mteule  wa Afya Susan Wafula anasema ana thamani ya Sh101 milioni.

Aliwaambia wabunge wanaowahoji Mawaziri wateuliwa Jumatano mali zake nyingi ziko katika mfumo wa ardhi iliyoenea katika kaunti nne.

"Thamani yangu ni takriban Sh101 milioni inayojumuisha nyumba ya mjini Syokimau na ardhi Kangundo. Nina ardhi Trans Nzoia, Bungoma, kaunti ya Kakamega," alisema.

Wafula alisema kuwa ana hisa na amana katika Waumini Sacco na UN Women saccco.

Wafula alizungumza alipofika mbele ya Kamati ya Bunge ya Kitaifa kuhusu Uteuzi katika Jumba la Kaunti, Nairobi.

Yeye ni miongoni mwa wagombea 22 wa Baraza la Mawaziri waliopendekezwa kuteuliwa na Rais William Ruto.