Ujumbe wa Kindiki kwa aliyekuwa waziri wa usalama wa ndani Matiang'i

Katika taarifa baada ya kutwaa mamlaka hiyo, Kindiki alimpongeza Matiang'i kwa utumishi wake.

Muhtasari
  • Mnamo Jumatatu tarehe 31, Kindiki alipokea kazi yake ya kwanza kutoka kwa Rais William Ruto
KITHURE KINDIKI AKIWA MBELE YA KAMATI YA USAILI YA BUNGE LA KITAIFA
Image: EZEKIEL AMINGA

Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki amechukua wadhifa rasmi.

Aliyekuwa waziri Fred Matiang'i alikabidhi ofisi kwa Kindiki Jumanne katika Harambee House.

Katika taarifa baada ya kutwaa mamlaka hiyo, Kindiki alimpongeza Matiang'i kwa utumishi wake.

"Ninamshukuru Dkt Fred Matiangi kwa utumishi wake kwa Taifa letu kama Waziri wa Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya Kitaifa. Ninamtakia kila la heri katika ziara yake ijayo," akatweet.

Mnamo Jumatatu tarehe 31, Kindiki alipokea kazi yake ya kwanza kutoka kwa Rais William Ruto.

Ruto aliagiza Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi (IPOA) kupea afisi ya Kindiki maelezo yanayohitajika kuhusu jinsi ya kukabiliana na mauaji ya kiholela.

Kindiki aliwahi kuwa Seneta wa Tharaka Nithi lakini hakuweza kuwania kiti chcochote katika uchaguzi uliopita.