Polisi Wapata Mifugo 700 Iliyoibiwa na Watu Wanaoshukiwa Kuwa Majambazi

Kulingana na polisi, jambazi mmoja alijeruhiwa vibaya huko Turkana huku mifugo hiyo ikirudishwa kwa wamiliki wao halali.

Muhtasari
  • Operesheni hiyo inajiri wiki moja tu baada ya Rais William Ruto kuagiza Kamishna wa Mkoa wa Rift Valley, Mohammed Maalim, kupeleka wanajeshi zaidi
Polisi Wapata Mifugo 700 Iliyoibiwa na Watu Wanaoshukiwa Kuwa Majambazi
Image: NPS

Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) imefanikiwa kupata zaidi ya mifugo 700 iliyoibwa katika maeneo yanayokumbwa na ujambazi katika Kaunti za Turkana, Isiolo, Pokot Magharibi, Samburu, Elgeyo Marakwet, Laikipia na Baringo.

Hatua za polisi, ambazo ziko chini ya Operesheni kubwa ya Komesha Uhalifu, ziliwezesha polisi kupata mbuzi 500, ng'ombe 70 na ngamia 200 waliokuwa wameibiwa katika maeneo hayo na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi.

Kulingana na polisi, jambazi mmoja alijeruhiwa vibaya huko Turkana huku mifugo hiyo ikirudishwa kwa wamiliki wao halali.

Operesheni hiyo inajiri wiki moja tu baada ya Rais William Ruto kuagiza Kamishna wa Mkoa wa Rift Valley, Mohammed Maalim, kupeleka wanajeshi zaidi ili kusaidia juhudi za askari wa akiba katika maeneo yaliyoathiriwa  ili kudhibiti tishio la ujambazi ambalo limegharimu maisha ya watu wengi.

"Askari wa akiba ambao kijadi wanatoka katika jamii za wenyeji wanachukuliwa kuwa ngome madhubuti dhidi ya majambazi na wezi wa ng'ombe kwa sababu ya ujuzi wao wa ardhi ngumu na mafichoni yanayotegemewa na wahalifu kufanya mashambulizi na kutatiza shughuli za usalama."

"Siku ya Jumatatu, timu ya usalama ilifanikiwa kupata ng'ombe 70 na mbuzi 150 baada ya makabiliano na kundi la washambuliaji waliokuwa wamejihami na kusababisha kifo cha angalau mshukiwa mmoja wau jambazi. hata hivyo imekuwa katika kaunti ya Isiolo ambapo ngamia 200 na mbuzi 300 waliokuwa wameibiwa walipatikana na kurudishwa kwa wamiliki."

Huduma ya polisi imewahimiza wananchi kutoa taarifa zozote kwa chombo cha sheria ambacho kinaweza kusababisha kukamatwa kwa watu wanaoshukiwa kuwa ni majambazi.