Bidhaa za nyama za Kenya kuruhusiwa nchini Afrika Kusini- Rais Ruto asema

Ruto mnamo Alhamisi alitangaza kuondolewa kwa marufuku ya miaka 10 ya bidhaa za nyama za Kenya

Muhtasari
  • “Hatuwezi kuuza chai yetu kwa Afŕika Kusini. Tuna changamoto ya kuuza mananasi na parachichi zetu
rais Ruto
rais Ruto
Image: FACEBOOK//RUTO

Rais William Ruto amesema kuwa kuanzia mwezi ujao Kenya itaanza kuuza bidhaa za nyama nchini Afrika Kusini kufuatia mazungumzo na rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa katika Ikulu ya Nairobi, Jumatano.

Ruto mnamo Alhamisi alitangaza kuondolewa kwa marufuku ya miaka 10 ya bidhaa za nyama za Kenya na nchi ya pili kwa uchumi barani Afrika, kuanzia Desemba.

"Jana, hatukufungua tu masuala ya usafiri, tuliondoa vikwazo….Tumekuwa na marufuku ya miaka 10 ya bidhaa zetu za nyama kufikia soko la Afrika Kusini. Tumejitolea na jana jioni tulipata taarifa fupi kutoka kwa mawaziri wanaohusika kuwa ifikapo Desemba mwaka huu, marufuku hiyo itaondolewa ili bidhaa zetu ziweze kupata soko la Afrika Kusini,” alisema rais.

Mkuu wa Nchi ambaye alikuwa akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chemba ya Kitaifa ya Biashara na Viwanda (KNCCI) jijini Nairobi alitaja kanuni za usafi wa mazingira kama sababu iliyofanya Afrika Kusini kuorodhesha bidhaa za Kenya.

Ruto alibainisha kuwa kanuni hizo pia zimeathiri mauzo ya Kenya ya mazao ya shambani kama vile majani chai na parachichi kwenda Afrika Kusini, lakini akasema kuwa serikali hizo mbili ziko katika harakati za kuoanisha mahitaji

“Hatuwezi kuuza chai yetu kwa Afŕika Kusini. Tuna changamoto ya kuuza mananasi na parachichi zetu

Suala lilikuwa tunafanya kazi kwa mahitaji tofauti ya usafi wa mwili. Tutaenda kuoanisha kanuni zetu za usafi wa mazingira ili ifikapo Januari tuweze kupata soko la Afrika Kusini wanapopata soko letu,” alisema.