Maajabu baada ya mvulana,15,kukwama akijaribu kuiba kwenye duka Machakos

Inaaminika kuwa kijana huyo alikuwa akivunja duka hilo kwa nia ya kuiba vyuma hivyo.

Muhtasari
  • Baadhi ya wakazi walidai huenda kijana huyo alikuwa pamoja na washambuliaji wengine, pengine watu wazima wakati wa kisa hicho
Crime Scene
Image: HISANI

Mvulana mwenye umri wa miaka 15 alikwama alipokuwa akijaribu kuvunja duka la chuma huko Tala, kaunti ya Machakos.

Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Matungulu Peter Omondi alisema kisa hicho cha Jumanne saa 3.00 asubuhi kiliripotiwa katika kituo cha polisi cha Tala.

"Alikuwa akijaribu kuiba katika duka la chuma kupitia tundu la kufuli la mlango. Hata hivyo, magunia yalimwangukia mkono huku mkono wake ukiwa bado ndani.

"Magunia yalikuwa mazito na hakuweza kuyaondoa, kwa hivyo alikwama hadi akaokolewa asubuhi," Omondi aliambia Star Jumanne.

Alisema kijana huyo anakosa mwongozo.

Inaaminika kuwa kijana huyo alikuwa akivunja duka hilo kwa nia ya kuiba vyuma hivyo.

Watu waliojionea walisema hawakuweza kumsaidia mvulana huyo kutoka nje ya mlango ambapo alikuwa amekwama. Alibaki akichuchumaa hadi asubuhi.

Baadhi ya wakazi walidai huenda kijana huyo alikuwa pamoja na washambuliaji wengine, pengine watu wazima wakati wa kisa hicho.

"Nashuku hakuwa peke yake, labda alikuwa na baadhi ya watu wazima waliokuwa wakimuelekeza na wakatoroka mambo yakiwa mazito. Hawezi kufikiria haya yote peke yake," mkazi mmoja alisema.